MWILI WA DKT. SENGONDO MVUNGI KUWASILI LEO
- Get link
- X
- Other Apps
Tume ya
Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za
kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki
nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili
nchini siku ya Leo.Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha,
siku ya Kesho, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa
4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya
Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16,
2013.
Aidha,
Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba
17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa
ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18,
2013.
Dkt.
Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya
Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili
ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili
(MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Wakati
huohuo, Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na
Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba 13, 2013)
wameungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt. Mvungi eneo la
Kibamba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu
na jamaa wa marehemu Dkt. Mvungi.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment