Mtuhumiwa sugu akamata mkoani Simiyu...Silaha 45 za kivita , 17 za kienyeji na risasi 892 zanaswa



OPERESHENI Maalumu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kukabiliana na vitendo vya Ujambazi, Ujangiri wa uwindaji haramu pamoja na wahamiaji haramu umefanikisha kukamatwa kwa silaha 45, zikiwemo za Kivita na 17 za kienyeji na risasi 892 na magazine 24 huku watuhumiwa sugu wa ujambazi na ujangiri wakitiwa mbaroni.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi.

Akizungumza jana na mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi alisema kuwa opresheni hiyo ilitokana na kuwepo vitendo vya uhalifu katika Wilaya tano za Mkoa huo na kwenye maeneo ya mbalimbai ya Mapori Tengefu ya Uwindaji kwa kipindi cha mwaka moja tangu kuanzishwa kwake Desemba 2012.

Silaha zilizokamatwa za kisasa na za kienyeji.

Kamanda Msangi alieleza kuwa miongoni mwa silaha hizo 45 na magazine 28 zilikamatwa ni pamoja na SMG 7 risasi 763 na G3 moja ikiwa na risasi zake 35 iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke mmoja aliyekamatwa Hollo Mabuga (28) mkazi wa Wilayani Bariadi, silaha nyingine 13 zilisalimishwa kwa hiali na baadhi ya watu waliokuwa wakizimiliki kinyume na sharia,Short-Gun saba, Gobole 17 na SAR moja.

Shehena ya risasi zilizo kamatwa.

“Tumeweza pia kumkamata mtuhumiwa hatari wa matukio ya uhalifu ambaye hivi karibuni aliachiwa kutoka Gerezani lakini tukapata taarifa za raia wema kuwa amekuwa akijihusisha na ujangiri na ujambazi ambaye ni Masanja Sumuni, tukaweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na SMG moja na risasi 96 huku mke wake Hollo Mabuga akikutwa pia na silaha” alisema.

Silaha za zilizotengenezwa kienyeji.

Kufatia operesheni hiyo Jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wane katika maeneo ya Wilaya ya meatu huku zaidi ya watu kumi waliokuwa wakijihusisha na ujangiri wakikutwa na nyara za serikali ikiwa ni za wanyama waliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mapori ya Akiba katika Wilaya za Meatu, Maswa na Itilima.

“Tumeunda kikosi kazi ambacho pia kinaendelea na operesheni ya kuwakamata wafugaji na mifugo yao ambao wamekuwa wakichungia mifugo ndani ya eneo la Hifadhi ya Serengeti ambapo zaidi ya ng’ombe wengi walikamatwa na kutozwa faini ambapo zaidi ya shilingi milioni 180 zilipatikana huku watu wanaoendesha vitendo vya ujangiri wakiuwa tembo na wamyama na kuuza kwa wananchi wa maeneo ya jirani” alisema Kamanda.

Kamanda Msangi amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za siri zitakazowawezesha kuwakamata wahalifu na wahamiaji haramu katika maeneo yote ya Wilaya za Meatu, Maswa, Bariadi, Itilima na Busega huku makakati wa kuanzisha vikosi kazi kila tarafa ukiwa mbioni kukamilika ili kuimalisha ulinzi kwa wananchi na mali zao.

source: GSENGO

Comments

Popular posts from this blog