DIAMOND PLATINUM ALIVYOPOKELEWA AIRPORT AKITOKEA CHINA
MSANII mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' leo ametua nchini akiambatana na ndugu yake pamoja na rafiki yake wakitokea nchini China. Msanii huyo pamoja na alioambatana nao, wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nane mchana ambapo wamelakiwa kwa shangwe na mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim 'Sandra'. Akiongea na Mtandao huu, Diamond ameeleza kuwa alienda nchini China kwa ajili ya mapumziko. Akiwa China, Diamond alikutana na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu 'Madam' na kuonekana wapo 'close' jambo lililoashiria kuwa wawili hao wamerudiana.
GPL
Comments
Post a Comment