MUUZA CHIPS AMTEKA MTOTO TANDALE DAR NA KUTOKOMEA NAE KUSIKOJULIKANA
MTOTO wa kike
mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar
es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na
kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe
shilingi milioni 6 ili amuachie.
Mama mzazi wa
mtoto aliyetekwa akiwa na
mwanaye.
Tukio hilo la kusikitisha
lilitokea Oktoba 16 mwaka huu baada ya kijana mmoja, anayefanya biashara ya
kuuza chipsi anayejulikana kwa jina la Issa Ramadhani, kudaiwa kumchukua mtoto
huyo aliyekuwa akicheza nyumbani kwao na kutoweka naye kabla ya wazazi wake
kubaini na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama
‘Mabatini’.Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi.
Mtuhumiwa wa
utekaji.
Wakizungumza na mwandishi
wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa polisi na kufunguliwa
jalada nambari KJM/RB/8994/13 baada ya kupashwa kuwa mtekaji ambaye alishaacha
kazi yake ya kukaanga chipsi, aliondoka muda mrefu na binti yao na hakukuwa na
dalili za kurejea.Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, wazazi hao pamoja na majirani walifanya uchunguzi wa chinichini na kufanikiwa kupata namba ya simu ya mtekaji huyo, lakini walifanikiwa kubadilishana naye ujumbe mfupi wa simu kwani hakuwa akipokea simu yake ya kiganjani.
Baba mzazi wa
mtoto aliyetekwa akiwa na
mwanaye.
Inadaiwa kuwa katika
mawasiliano hayo, mtekaji alikataa katakata ombi la kumtaka amrudishe mtoto wao
na kutaka apewe kiasi cha shilingi milioni 6 ili kutekeleza jambo hilo ingawa
baadaye ilibainika jamaa huyo alikuwa Gairo mkoani
Morogoro.Wazazi hao walisema kuwa Oktoba 19 mwaka huu mmoja wa majirani walioguswa na tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Justin Henry alijitolea kusafiri mpaka Gairo kumsaka mtoto na mtekaji wake jambo ambalo lilifanikiwa kwa kumpata mtoto akiwa mzima wa afya japokuwa mtekaji alishtukia na kukimbia.
Comments
Post a Comment