AMREF YAANDAA CHAKULA CHA HISANI KUCHANGISHA FEDHA ZA KAMPENI YA “STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS”



pic 2Mkurugenzi wa Taasisi ya AMREF Tanzania Dk.Festus Ilako akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda  na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dk, Rita Noronha.
pic 4Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda  akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo imeandaliwa na AMREF wakishirikiana na Montage itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam.

pic 6Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya AMREF Tanzania Dk.Festus Ilako leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea nao  kuhusu  halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)

………………
Eleuteri Mangi-Maelezo
TAASISI ya AMREF Tanzania imetangaza inatayarisha chakula cha hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuwasaidia akina mama na watoto itakayokuwa na kauli mbiu “Satand for African mothers“ mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dr. Festus Ilako alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
“Fedha zitakazochangiwa zitakuwa kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuwasaidia akina mama na watoto ili kupunguza vifo vya wanawake na watoto” alisema Dr.Ilako.
Dr. Ilako alisema kuwa hafla hiyo itafanyika Oktoba 11, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo taasisi yake inashirikiana na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Milenia ya kuboresha huduma za afya hasa za akina mama na watoto.
 Dr. Ilako alisema “ili kufikia malengo hayo, kunahitajika kuwa na wakunga wa kutosha kuimarsha Nyanja ya uzazi salama kufanikisha malengo ya millennia”.
Dr. Ilako alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kujitokeza siku hiyo na kujitolea katika kuchangisha fedha ili kufikia malengo ya ya kutoa elimu kwa wakunga 3,800 ifikapo 2015.
Tangu kampeni hiyo ianzishwe tayari wakunga 10 wamewezeshwa kupata elimu na wengine 70 wategemewa kujiunga.
Ili kufanikisha malengo kuboresha huduma ya mama na motto kunahitajika uboreshaji wa ujuzi wa wakunga 2800 kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya “e-lerning “na kutoa mafunzoya awali kwa walau wakunga 1000 mpaka mwaka 2015.
Mkurugenzi huyo aliitaja mikoa inyonufaika na mpango huo ni mpaka sasa ni Tanga, Mtwara na Simiyu na kuainisha kuwa lengo la taasisi yake ni kiifikia mikoa yote ya Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Tanzania Teddy Mapunda  alisema kuwa wanatarajiwa kuhudhuria ni pamoja na viongozi wakuu wa taasisi mbalimbali  za kiserikali, za binafsi ndani na nje ya nchi na wananchi wote
Mapunda pia aliwaomba vyombo vya habari kuwa mabalozi wazuri ili watanzania wajue AMREF inafanya nini ili watanzania waweze kuwa na uzazi salama.
Kufanikisha azma hiyo Mapunda aliwaomba watu wote wenye mapenzi mema kutoa  michango yao na kuisilisha kupitia huduma ya M-pesa kwa namba 0752-167286, au akaunti ya NBC makao makuu, 0111030004548 ama kununua meza ya watukumi katika hafla hiyo  kwa kiasi cha dola 1500 sawa na shilingi 2430000 za kitanzania.   
Kampeni ya “Stand up for African Mothers” ilizinduliwa mwaka 2012 ambapo  AMREF ina zaidi ya miaka 57 katika kutoa huduma za kijamii sehemu mbalimbali.
Wadhamini wa hafla ya kuchangisha fedha hiyo ni  banki ya AMREF ikishirikiana na benki ya NBC, Serengeti  Breweries  na ITV. 

Comments

Popular posts from this blog