WEMA SEPETU ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMTUKANA MENEJA WA HOTELI WAKATI POMBE IKIWA UTOSINI



DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo  iliyopo Kawe Beach, jijini Dar.



Akizungumza na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.

Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika  saa tano usiku, Wema na marafiki zake  walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.


Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.


Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?.
 
Aliongeza kuwa swali lake kwa kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii.


“Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.”
 
Faili la kesi hiyo linasomeka KW/RB5988/2013, SHAMBULIO.

Comments

Popular posts from this blog