Posts

KAJALA ANAPATA WAPI JEURI HII?

Image
Imelda mtema FEDHA inaongea! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji Kajala Masanja kupanga kwenye mjengo mpya wa maana na kuushehenesha samani na ‘vikorombwezo’ kibao hadi kufikia hatua ya watu kuhoji, amepata wapi jeuri hiyo ya fedha? Ijumaa limenasa mchapo kamili. Mjengo anaoishi mwigizaji Kajala Masanja. Kajala ambaye awali alikuwa akiishi maeneo ya Sinza-Madukani, kwa sasa amehamia katika mjengo huo mpya uliopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo, ndani ya mjengo huo, Kajala anaishi na mwanaye Paula huku akiwa amewaajiri wafanyakazi wa ndani watatu na kulindwa na kampuni maalum ya ulinzi. “Yani Kajala ananuka hela. Mjengo wake mpya una kila kitu ndani. Ukiingia unaweza kupagawa kutokana na vitu vilivyomo ndani. Watu tunajiuliza ni nani anayempa jeuri hii maana filamu pekee haziwezi kufanya matusi haya,” kilisema chanzo hicho. ...Sebuleni. Baada ya kupenyezewa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alitia timu nyumbani hapo kwa Kajala na kuji

SIASA MWAKA HUU VITA NZITO!

Image
Imelda Mtema Nivita nzito! Wakati mtifuano wa mastaa wawili wa kike wa sinema za Kibongo ambao huko nyuma walikuwa wakipigia kampeni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Jacqueline Wolper Massawe na Aunt Ezekiel Grayson ukiwa umekolea, kumeibuka balaa lingine la mastaa wawili wa kiume wa tasnia hiyo, Jacob Steven ‘JB’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wanaodaiwa kuzichapa laivu.  Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe. AUNT AANIKA SIRI ZA WOLPER UKAWA Katika sakata lao, Aunt anadaiwa kuanika siri za Wolper mara tu baada ya kung’atuka Ukawa akiwa na mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ ambao wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wakati anatimkia CCM mapema wiki hii, Aunt aliliambia gazeti hili kuwa ameamua kuondoka Ukawa kwa kuwa sera za CCM zimemshawishi na kwamba mwanzoni alipotea na kwamba hahitaji mabadiliko badala yake anataka kuchapa kazi kama ilivyo kaulimbiu ya mgombea wa urais wa CCM, Dk.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC,YAAHIDI KUMTANGAZA LOWASSA MAPEMA BAADA YA KUSHINDA!!

Image
Na Neophitius Kyaruzi TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imevitaka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuachana na dhana kuwa mgombea wa Chadema anayeungwa mkono na umoja huo hatatendewa haki na tume huku ikiahidi kwamba atatangazwa mapema iwapo atafanikiwa kushinda. Ufafanuzi uliotolewa juzi na baadhi ya wanasheria wa tume hiyo katika mahojiano maalum na gazeti hili, unasema kuwa tume hiyo inaendeshwa kwa misingi ya sheria na maadili ya uchaguzi wa rais, wabunge na maadili ya mwaka huu, hivyo watarajie kuwa na uchaguzi huru na wa haki unaosimamia misingi hiyo. “Tunajua baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakieneza maneno kuwa NEC haitatenda haki kwa baadhi ya wagombea lakini niseme tu kwamba tume hii haiendeshwi kwa misingi ya matakwa ya watu fulani bali ni chombo cha kisheria hivyo kinafanya kazi katika misingi hiyo na kamwe hakitapendelea mwanasiasa au chama chochote badala yake kitatenda haki,” alisema mwanasheria wa tume hiyo, (jina tunalihifadhi kw

James Mbatia Kuhamia Chadema...NCCR Mageuzi Wadai Amekuwa Msemaji wa Chadema Badala ya Kujenga Chama

Image
Mbatia na Lissu Kuna kila dalili kuonyesha mbatia atakihama chama chake kwenda Chadema. karibuni akionekana kua msemaji wa mambo ya Chadema hadi kuwashangaza wafuatiliaji wa mambo ya siasa. sasa amejitenga na viongozi wenzake wa NCCR Mageuzi hadi wanatishia kujitoa UKAWA.. ameshindwa kutetea maslahi ya NCCR ndani ya UKAWA na inaekekea amelewa mahaba ya Lowassa mtu anayedaiwa kua tajiri sana. Je Mbatia naye atakua nyumbu kufuata malisho Chadema? si siku nyingi tutapata jibu. Sumaye ambanae inasemekana amejiunga na NCCR japo hakuna ushahidi wa kukabidhiwa kadi ameoneka na jezi ya CHADEMA kwenye mikutano akipiga debe kwa Lowassa. ni wazi NCCR ni mwathirika wa UKAWA na itabaki na ukiwa. inaelekea nyumbu wote watafuata alipo EL. alipo Edo nyumbu wote wapo. tuombe mungu apishilie mbali UKAWA kutwa uongozi ama sivyo tutaona mparurano wa kugombea vyeo.. Sumaye tayari amapewa uwaziri mkuu mbowe inasemekana atakabidhiwa hazina! mbatia bado haifahamiki etc By Kmbwembwe

WANAHITAJIKA VIJANA 120 KUJAZA NAFASI ZIFUATAZO ZA AJIRA SERIKALINI

Image
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA Kumb. Na EA.7/96/01/H/67 15 Septemba, 2015 TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma). Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 120 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili. NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE. i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa. iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia s

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 18.09.2015

Image

MSAFARA WA SUGU WASHAMBULIWA KWA MAWE AKIELEKEA KATIKA KAMPENI ZAKE ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA

Image
Gari la Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Sugu likiwa kituo cha Polisi kati jijini Mbeya mara baada ya kushambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM Sugu akiwa kituo cha Polisi na wafuasi wake.Picha Kenneth Ngelesi Mbeya . (JAMIIMOJABLOG MBEYA ) Na Emanuel Kahema ,Mbeya MGOMBEA ubunge  kupitia chadema jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi leo  amejikuta katika wakati mgumu baada ya msafara wake kushambuliwa na mawe na wafuasi wanaosadikiwa kuwa ni wa chama   cha mapinduzi CCM na kwamba katika tukio hilo watu wawili wamejeruhiwa akiwemo dereva aliyekuwa akimuendesha mgombea huyo  . Tukio hilo la kushambuliwa kwa msafara huo, limetokea majira ya saa 11 za jioni katika eneo  la barabarani lililopo katika Kata ya Ghana mtaa wa Mbata jijini hapa  ambapo inasemekana mgombea huyo alikuwa  katika harakati za kampeni kuomba kura kwa wananchi wa Iziwa  ambapo mgombea huyo alikuwa ndani ya gari yake yenye namba za usajili T161 CP

MO DEWJI ANYAKUA TUZO YA MWAKA YA MFANYABIASHARA ANAYESAIDIA ZAIDI JAMII

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker akimkabidhi tuzo ya '2015 Philanthropist of the year-East Africa' Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji katika sherehe zilizofanyika hoteli ya DusitD2 jijini Nairobi.(Picha zote na Zainul Mzige wa  Modewjiblog ). Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akizungumza kwenye hafla ya tuzo za All Africa Business Leaders Awards 2015 (AABLA). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker. Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akipozi katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker.   Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ameshikilia tuzo yake. Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa jijini Nairobi ambapo pia walimpongeza. Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohamme

RAIS KIKWETE AZINDUA MAJENGO PACHA YA GHOROFA 35 YA PSPF TOWERS MTAA WA SOKOINE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw.  Adam Mayingu alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015  Mrisho Mpoto na Mjomba Band wakitumbuiza kwenye sherehe za  majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr. Ramadhani Dau   alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015   majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam yaliyozindulia  leo Septemba 16, 2015   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF  Mkurugenzin Mkuu  wa  Mfuko  wa  Pensheni  wa PSPF , Adam Mayingu katika sherehe za kuzindua majengo pacha ya ghorof