MTOTO APIGWA KIKATILI NA BABA'AKE..AFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA!
Mtoto Amani Elisha (10) aliyepigwa vibaya na baba yake mzazi hadi kuzimia kwa siku mbili. KATIKA hali ambayo siyo ya kawaida iliyowashangaza wakazi wa eneo la Ukonga Mazizini kwa Makobe, baba mmoja aliyefahamika kwa jina la Elisha Zakari amedaiwa kumpiga mwanaye wa kumzaa kip i go kama cha ng’ombe machungani na kusababisha azimie na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto huyo aliyepigwa ni Amani Elisha (10) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maarifa iliyoko Ukonga, Dar es Salaam, baada ya kipigo alizimia siku mbili. Tukio hilo la kikatili lilitokea usiku wa Ijumaa iliyopita na sababu ya mtoto huyo kupewa kipigo inadaiwa ni kutokana na utoro shuleni na kwamba hata akienda huwa haandiki.Waandishi wetu waliponasa tukio walimtafuta mama mzazi wa mwanafunzi huyo maarufu kama mama Amani na mahojiano yakawa hivi: Mwandishi: Mama ni kweli kuwa mume wako alimpiga mtoto wenu? Mama Amani: Ni kweli baba yake Amani ndiye aliyempi...