Makubwa yameibuka baada ya msanii Steven Mengere āSteve Nyerereā, kufungua kinywa na kusema kuwa ugonjwa wake si bure bali amepigwa kipapai. Akizungumza na mwandishi wetu,Steve alisema kuwa kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa ajabu kwa kipindi kirefu sasa na madaktari kushindwa kuelewa kila walipompima, staa huyo anaamini kuwa amerogwa na msanii mwenzake. āNimetembea kwa wataalamu wa mambo ya asili na kugundua hilo, sasa ninalazimika kuamini katika imani za kishirikina ingawa ni kitu ambacho muda mrefu nilikuwa nikikipinga sana lakini kwa hili ninaamini kweli nimechezewa na ndiyo maana niko hivi hadi sasa,ā alisema Steve bila ya kupepesa macho. āNashindwa kumtaja mhusika wa tukio hili kwa sasa ila mwenyewe atakuwa anajua ni kwa kiasi gani nimemgundua, nimejua kwamba wasanii hatupendani hata kidogo na wala hakuna anayependa mafanikio ya mwingine. āIpo siku nitamtaja ila leo ngoja niishie kusema kwamba nimechezewa na namshukuru Mungu kw...