Rais Magufuli atoa Shilingi milioni 100 kumtibu Mgunduzi wa Tanzanite

Leo April 6, 2018 Rais John Magufuli katika Uzinduzi wa Ukuta wa Mirerani amesema serikali yake itatoa kiasi cha Shilingi milioni 100 kwa ajili ya matibabu ya Mzee Jumanne Ngoma ambaye ndiye mgunduzi wa madini ya Tanzanite.
Rais Magufuli ameeleza kuwa serikali inatoa pesa hiyo ili Mzee Ngoma ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kupooza akapatiwe tiba kwani ugunduzi wake ndio ulioweka historia ya nchi ya Tanzania kumiliki madini hayo.

Takriban mwezi mmoja uliopita Mzee Ngoma alifanyiwa mahojiano na Ayo TV na millardayo.com na kueleza kuwa anatamani kuonana na Rais Magufuli ili amueleze adha anayokutana nayo na jinsi ambavyo kuona hathaminiwi wala kunufaika na chochote licha ya ugunduzi alioufanya.
Mzee Ngoma anadaiwa kugundua madini hayo miaka 52 iliyopita.

Comments

Popular posts from this blog