Breaking News: Wambura Ashindwa Rufaa Yake, Ataendelea na Kifungo
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura.
Kamati Ya Rufaa Maadili Ya TFF baada ya kupitia rufaa ya aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo,Michael Richard Wambura imetupilia
madai yake yote na adhabu yake itaendelea kama ilivyoamuliwa na Kamati
ya Maadili ya TFF kwa kufungia kutojihusisha na soka maisha yake yote.Mbali na hilo pia kamati hiyo ya rufaa imeshauri, Wambura afikishwe kwenye vyombo vya dola ili suala hilo liweze kushughulikiwa zaidi na wataalam
Comments
Post a Comment