Athari Zitokanazo Na Msongo Wa Mawazo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nazo

Watalamu wa masuala ya saikolojia wanasema ya kuwa kila binadamu, huwa na msongo wa mawazo, hii ni kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha ikiwemo na changamoto za kimahusiano, na mambo mengine mengi.

ATHARI ZITOKANAZO NA MAWAZO (STRESS)
1. Kuwa na mawazo husababisha mwili kuwa dhoofu, pia muda mwingine kuweza kusababisha magonjwa mengine.

2. Kupatwa magonjwa ya shinikizo la moyo, ni sababu tosha kwamba chanzo chake ni msongo wa mawazo.

3. Kuharibika kwa nywele ikiwa ni pamoja na kukatika kwa nywele hivyo unapoona nywele zako hazikui vyema wakati unazihudumia vizuri, tatizo huweza kuwa ni hilo la msongo wa mawazo pia.

4. Akili kushindwa kufanya kazi vizuri.

Njia za kuondoa msongo wa mawazo

1. Kukwepa vyanzo vya msongo wa mawazo:- Usipende kukaa na wanaokusababaishia ama kukupa msongo wa mawazo, tafuta mazingira mengine tofauti na hayo.

2. Badilisha mazingira:- Hii inaweza kukusaidia kwani itaupa nafasi ubongo wako kufikiri mawazo mengine mapya. Wengine hupendelea kutembelea sehemu tofauti kama kusafiri.

3. Pumzisha na burudisha mwili wako:- Unaweza kupumzisha mwili kwa kusikiliza muziki ama kuangalia vipindi vya kukuburudisha mfano vichekeosho.

4. Mazoezi na chakula kizuri:- Hakikisha unapata chakula kizuri na kinachokupendeza (unachokipenda) ila zingatia mlo kamili na pendelea kufanya mazoezi  mepesi.

Comments

Popular posts from this blog