STAA ZARI AMJIA JUU HAMISA.

Bado majina ya baby mama’s wake Diamond Platnumz yanazidi kuchukua headlines kila kukicha katika mitandao ya kijamii, ambapo Zari na Hamisa Mobetto wamekuwa wakirushiana vijembe katika mitandao ya kijamii toka Zari afahamu kuwa Hamisa amezaaa na Diamond.

Zari anaonekana kuendelea kurusha vijembe kupitia instagram yake na kujiita kuwa yeye ni mchepuko wa Diamond Platnumz kutokana na vijembe ambavyo Hamisa Mobetto alivirusha kwake siku chache zilizopita, Kupitia mtandao wa snapchat wa Zari alipost picha 7 ambazo kwa kila picha alindika caption na kusemekana kuwa kwa kile alichokiandika amemjibu Hamisa Mobetto juu ya vijembe vyake.
“mdogoo, kila siku mdogo!! Mdogo na mzuri lakini huwezi kupata mwanaume wako….mwanamke gani haujiamin……kama unajiamini na uzuri na akili basi tuone ni mwanaume gani atakutaka baada ya hizi drama….baba wa mtoto wa tatu anakuja na atakuacha tu”
“unaweza kuendele kupost picha zako za zamani na kila kitu nimetengeneza amani na makosa yake, siwezi kubadilisha ya nyuma nimetengeneza amani na ninatengeneza maisha yangu ya mbeleni”
“kila mtu hapa anaongelea karma ulijua kabisa ni mwanaume wa mtu na anafamilia lakini ukampanulia miguu yako na kupata mimba unahisi karma itanirudia?? Nimefanya nini?? karma itakurudia wewe mpenzi mimi sijafanya kitu”

Comments

Popular posts from this blog