YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA BAADA YA VIKAO VYAKE KUANZA LEO
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika
Viwanja vya Bunge kwa ajili ya kushuhudia kiapo cha Mke wake Mama Salma
Kiwete aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuwa Mbunge.
Mbunge wa
kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiwasili katika viwanja vya Bunge Mjini
Dodoma kwa ajili ya kula kiapo na kuanza majukumu yake.
Mbunge wa
kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akisindikizwa na wabunge wanawake kwenda
kula kiapo cha kutumikia kazi yake leo Bungeni Mjini Dodoma.
Mhe. Salma Kikwete akila kiapo cha kuwa mbunge mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo bungeni Mjini Dodoma.
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao
cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki
akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano
wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijibu
hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba
wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu hoja mbalimbaliz za
wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini
Dodoma.
Mke wa
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akisalimia wabunge
mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni wa Spika leo Bungeni Mjini
Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mama Devotha Gabriel.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na Watu wenye Ulemevu
Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu cha Bunge kwa kuomba Bunge
kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za kazi kuendelea kwa
awamu ya pili saa kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifuatilia shughuli za Bunge leo Mjini Dodoma.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Comments
Post a Comment