MSANII YUSUPH MLELA ATOA MANENO HAYA KWA WASANI WENZAKE

Msanii mkongwe wa filamu Yusuph Mlela amewataka wasanii wenzake wa filamu kuacha kulalamika na kufanya kazi kwa bidii kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuikomboa tasnia ya filamu.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Mlela amedai kuwa wasanii wengi wanatakatamaa kwa kauli ya soko limeyumba wakati wao ndiyo watu pekee ambao wanaweza kuikomboa tasnia ya filamu.
“Suala la soko wadau wanasema limeyumba, lakini naweza kusema huu ni wakati wa kuamka na kuanza kufanya kazi upya kulikomboa soko la filamu, kama wanasema kazi ni mbaya tufanye kazi nzuri, kila kitu tunaweza kufanya. Mimi nadhani huu ni wakati wa wasanii wa filamu kuamka na kufanya kazi kwa bidii ili kuirudisha ile hali ya zamani,” alisema Mlela.
Muigizaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri ndani ya tamthilia ya Kashfa inayorushwa na Azam TV, anajipanga kuachia filamu yake mpya ‘Mr Bodaboda’ Machi mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog