Utafiti : MIMBA HUBADILISHA UBONGO WA MWANAMKE
Watafiti
wanasema mwanamke anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni ya oestrogen
huongezeka sana na pia mwili wake kubadilika hata hivyo, si wataalamu
wengi walikuwa wamechunguza mabadiliko kwenye ubongo.
Watafiti
kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na
Leidenwalichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi
baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye
ubongo. Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature
Neuroscience.
Wanasayansi
hao wanasema ujauzito hupunguza seli za ubongo katika baadhi ya sehemu
za ubongo wa mwanamke ili kumuwezesha kuhusiana vyema zaidi na mtoto na
kujiandaa kwa majukumu yake kama mama ambapo hubadilisha ubongo wa
mwanamke kwa kipindi cha hadi miaka miwili.
Uchunguzi
ulifanywa kwa wanawake 25 waliokuwa wameshika mimba kwa mara ya kwanza
ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka miwili
baada ya mwanamke kujifungua.
Watafti
hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika kipindi
hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo, lakini hata hivyo,
hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka
kumbukumbu.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment