WANAUME WAANZA KUHASIWA KENYA...150 WAMEJIANDIKISHA KUKATWA MIRIJA YA UZAZI
Shughuli
ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa
moja kutoka chumba cha upasuaji kutoka mjini Nairobi, Kenya kama njia ya
kuhamasisha watu kuhusu njia hiyo ya kupanga uzazi .Takriban wanaume
150 walijiandisha kufanyiwa shughuli hiyo iliyochukua muda wa takriban
dakika 20.Madaktari walifanya shughugli hiyo nyuma ya jukwaa lilifunikwa
katik ukumbi wa sanaa mjini Nairobi.Wamaume nchini Kenya ambao mara
nyingi wana hofu ya kufanyiwa zoezi hilo la kupanga uzazi mara nyingi
uhofia kunyanyapaliwa..
Wale wanaoendesha kampeni ya zoeizi hilo wanasema kuwa ndiyo njia salama ya kupanga uzazi.
"Wanaume
wengi hudhani kuwa zoezi hilo humnadili mwananamme kuwa mwanamke," Jack
Zhang ambaye ni daktari kutoka Canada aliiambia BBC.
Baadhi ya
wanaume wana hofu kuwa watu hufa kwa wingi barani Afrika kwa hivyo kuna
haja ya kuzaa watoto wengi.Mwandishi wa BBC mjini Nairobi, anasema kuwa
baadhi ya wanaume walishiriki zoezi hilo baada ya kuchochewa na gharama
ya kulea familia kubwa.
"Mbinu
ambazo mke wangu alikuwa akitumia kupanga uzazi, zilikuwa na madhara
kwake, kwa hivyo mimi niliamua kwenda kukatwa mirija ya ya uzazi,"
mwanamme moja aliiambia BBC.
Chanzo-BBC
Comments
Post a Comment