DC Hapi Atembelea Wajasiriamali Wa Airtel Fursa
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally
Hapi akikagua bidhaa za wajasiriamali wadogo waliowezeshwa kupitia
mpango wake wa Airtel Fursa. Kulia aliyeambatana naye ni Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano.
…Hapi akipata maelekezo ya changamoto
mbalimbali zinazowakabili kutoka kwa mjasiriamali aliyewezeshwa na
Airtel Fursa (aliyeko kulia).
…Hapi akiendelea kukagua nembo za TBS
na Bar Code katika bidhaa za wajasiriamali hao waliowezeshwa na mpango
mkakati wa Airtel Fursa.
…Hapi akikabidhiwa keki na Diana
Moshi aliyokuwa ameiandaa (kushoto) ambaye ni mjasiriamali anayemiliki
kampuni yake iitwaye Diana’s Oven aliyowezeshwa na Airtel Fursa.
Mjasiriamali wa kuchora aitwaye,
Theresia Deus (kushoto) akimuonyesha bidhaa zake mkuu huyo baada ya
kuwezeshwa Laptop kwa ajili ya kuchorea na Airtel Fursa miezi mitano
ilyopita sasa.
Hapi na RPC wa Kinondoni Suzan
Kaganda wakiangalia mayai ya kienyeji kutoka kwa mjasiriamali wa kufuga
kuku wa Wilaya ya Kibaha- Pwani aliyewezeshwa na Airtel Fursa.
Hapi akizungumza jambo baada ya kutembelea mabanda ya wajasiriamali hao.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano akizungumza jambo katika hafla hiyo.MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi leo ametembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Simu za Mikononi ya Airtel na kujionea mabanda ya shughuli mbalimbali za wajasiriamali waliowezeshwa na kampuni hiyo kupitia mradi wa Airtel Fursa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano alisema kuwa wajasiriamali hao waliofika kwenye viwanja hivyo ni wadogo na ni wale walioonyesha jitihada za kujikwamua kiuchumi na kuwezeshwa na mradi wao uitwao Airtel Fursa ili kujikwamua na umaskini kwa kuwawezesha kupata mitaji na vifaa vya kutimiza ndoto zao.
Aliongeza: “Mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali ni sehemu ya mpango wa Kampuni ya Airtel ili kuboresha maisha yao na ya watu wanaowazunguka.
“Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tuliona ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa,” alisema Singano.
Naye DC Hapi amesema kuwa Airtel wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kufanikiwa kuwawezesha wajasiriamali hao katika kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.
Alisema si tu kusubiri kuajiriwa katika taasisi binafsi au serikali bali inapaswa kuthubutu na kuanzisha mradi ili kuweza kuondokana na changamoto zinazoweza kukwamisha maendeleo.
Na Denis Mtima/Gpl
Comments
Post a Comment