Zari, Mobeto Kimenuka Tena!
Mwanamitindo Hamisa Mobeto.
DAR ES SALAAM: Kimenuka
tena! Ndiyo unavyoweza kusema baada ya mzazi mwenza wa staa wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss
Lady’ kutupia picha ya hereni kwenye Mtandao wa Kijamii wa Snapchat huku
akitupa dongo kwa kusema aliyesahau vitu vyake aende akavitoe, bifu
limeibuka upya mitandaoni.
Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Baada ya kutupia picha ya Snapchat hiyo,
mashabiki mbalimbali wa mtandao huo walijiongeza na kuoanisha na picha
ya Mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa kufananisha hereni alizovaa siku za
nyuma zikifanana na hizo alizodai Zari zimesahaulika kwenye chumba cha
Diamond, nyumbani kwake, Tegeta-Madale jijini Dar.
Mbali na mashabiki hao kujiongeza, mjadala mzito uliibuka pia
wakidai ugomvi wa Zari na Mobeto si rahisi kumalizika maana kati yao
hakuna anayeweza kuwa mpole na kumwachia mwenzake atambe. “Hili lazima
ni dongo kwa Mobeto, yaani hawa, hauwezi kupita muda hawajazinguana,
kweli mapenzi yanauma lol…” aliandika mmoja wa mashabiki wanaotumia
mtandao huo wa Snapchat.Staa wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zari .
Mjadala ulikuwa mkubwa huku kila mmoja
akimtetea anayempenda hadi mashabiki hao kufi kia hatua ya kutukanana
mitandaoni. Kuna ambao walimtetea Zari lakini wengine walikuwa upande wa
Mobeto.
Risasi Jumamosi lilimtafuta mwanamitindo huyo ili aweze kufungukia
hayo madai ambapo alisema ameziona lakini hakutaka kufunguka kama ni
zake au la: “Nimechukizwa na kitendo hicho. Kitendo hicho kimenifanya
mimi nitukanywe sana matusi ya nguoni kwenye mitandao ananitafuta sana
Zari lakini ipo siku atanipata,” alisema Mobeto. Hii si mara ya kwanza
kwa wawili hao kuingia kwenye bifu ambapo inadaiwa penzi la Diamond
ndilo linalowatia ‘uchizi’ hata kuwafanya w a k w a r u z a n e k i l a
mara
Comments
Post a Comment