WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI MAOFISA MISITU WANNE, APIGA ‘STOP’ UVUNAJI MAGOGO RUFIJI
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Maofisa Misitu wanne na
kusimamisha shughuli za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Rufiji kwa
muda usiojulikana baada ya kutoridhishwa na usimamizi wake.
Maofisa
waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira Dk. Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa
Misitu Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa
wilaya Seleman Bulenga.
Waziri
Mkuu amefanya uamuzi huo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati
akizungumza na watumishi wa wilaya ya Rufiji kwenye ukumbi wa
halmashauri kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
kwenye viwanya jumba la maendeleo wilayani Rufiji.
Aidha,
Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Njwayo kukusanya magogo
yoye yaliyoko msituni na kuyapiga mnada na kuitaka wizara ya Maliasili
na Utalii kwenda wilayani Rufiji kufanya uchunguzi wa leseni za uvunaji
walizozitoa kwa wilaya hiyo.
Waziri
Mkuu amebainisha kwamba wilaya ya Rufiji ni moja kati ya wilaya
inayoongoza kwa uvunaji wa mazao ya misitu bila ya kufuata taratibu
licha ya kuwa na maofisa misitu.
“Hakuna
mafanikio katika sekta ya misitu kwenye wilaya hii ya Rufiji.
Nasimamisha shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu pamoja na
watendaji wake kwa sababu hatuwezi kuacha watu wanakata magogo bila ya
kufuata taratibu,”
“Haiwezekani
Rufiji iwe shamba la bibi, nimesimamisha uvunaji wa magogo hata kwa
wenye leseni hadi tuzichunguze zimetoka wapi. Hatuwezi kuruhusu maofisa
wanashiriki vitendo vya hujuma kwa kuvuna misitu Rufiji na kugonga
mihuli ya Kilwa kisha fedha wanatia mifukoni,” amesema.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo
Rashid Salum kufuatilia maagizo aliyoyatoa kuhusu kizuizi cha Ikwiriri
kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipokutana na
watumishi wa wizara hiyo.
Julai 18
mwaka huu Waziri Mkuu alikutana na watumishi wa wizara hiyo jijini Dar
es Salaam na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa
na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji.
Waziri
Mkuu aliitaka wizara hiyo kupunguza idadi ya vizuizi vya ukaguzi wa
mazao ya misitu kwenye barababara mbalimbali baada ya kukosa tija,
alitoa mfano wa barabara ya kwenda mikoa ya kusini kuanzia Dar es
Salaam yenye vizuizi visivyopungua sita na kila kizuizi kinatumika kwa
ajili ya kukagua mazao ya misitu na maliasili inayotoka kuvunwa.
Awali
mbunge wa Rufiji Mohammed Mchengelwa alilalamikia vitendo vya dharau
vinavyofanywa na watumishi wa sekta mbalimbali katika wilaya hiyo jambo
linalosababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 26, 2016
Comments
Post a Comment