LOWASSA AISIFU SERIKALI URATIBU MAAFA KAGERA
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na
Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu alipomtembela leo ofisini
kwake kumpa pole kutokana na athari ya tetemeko la ardhi katika mkoa
wake
Na Mwandishi Wetu-KAGERA.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna
ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea
mkoani humo.Bw. Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa
pole kutokana na athari zilizotokana na tetemeko hilo.“Napenda
nikupongenze mkuu wa mkoa kwa namna ulivyokabili tukio hili, wala
hatukuwa na mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwa hiyo
jambo hili limempata mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja
mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.
Adha Mhe.
Lowassa alisema kuwa suala hili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali
peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa
hivyo watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.
Katika
kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko
400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea
kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na
serikali katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo
“Tunashukuru
watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia
waathirika wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele
kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema Meja
Generali Salum Kijuu.
Comments
Post a Comment