Fiesta Yawapagawisha Wabunge Na Mawaziri Dodoma











Mmoja wa mashabiki aliyejishindia moja ya zawadi (T-shirt) kutoka kwa waandaaji wa tamasha hilo.
DODOMA, Usiku wa kuamkia jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
kulifanyika tamasha la Fiesta ambako mamia wa wakazi wa manispaa ya
Dodoma na vitongoji vya jirani walihudhuria onesho hilo wakiwemo pia
baadhi ya waheshimiwa wabunge na mawaziri wa serikali ya tano
wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mheshimiwa
Nape Nnauye.Baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria tamasha hilo ni pamoja na William Ngeleja, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, Venance Mwamoto pia alikuwepo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Attickson na Waziri January Makamba.
Tamasha hilo lilivunja rekodi baada ya kuhudhuriwa na mashabiki wengi na kuacha historia ndani ya viunga hivyo yalipo makao makuu ya nchi yetu.
Wasanii wote walioshiriki kwenye tamasha hilo walifanya ‘show’ kali iliyowapagawisha mashabiki wao na kufanya tamasha hilo liwe la kipekee.
Imeandaliwa na Leonard Msigwa/GPL.
Comments
Post a Comment