WACHEZAJI NETBALL TANZANIA WAPEWA MEDALI ZA DHAHABU
Nahodha
wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ Dorita Mbunda akivalishwa medali na
Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada
ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa
Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi)
Kikosi
cha Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ katika picha ya pamoja na Viongozi wa
Timu hiyo muda mchache baada ya kuvalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la
Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua
ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali
Rwanda( Picha na Dora Mushi)
Kikosi
cha Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ kikiingia kuvalishwa medali na Mkuu
wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya
kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa
Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi)
Mkuu
wa Msafara wa Timu ya Tanzania Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba
(katikati) akiongea na Mchezaji Nasra Suleiman aliyeshika Tuzo ya MVP na
mwanaidi Hassan mara baada kuvalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga
wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa
Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda.
Mchezaji
wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ Nasra Suleiman akipokea kikombe cha
MVP na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba
baada ya Timu yake pia kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki
katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Selemani Semunyu).
Na Selemani Semunyu JWTZ
Wachezaji
wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ wamekabidhiwa Medali za Dhahabu ikiwa
ni sehemu ya kunyakua ubingwa wa Mchezo huo katika mashindano ya majeshi
kwa nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Kigali Nchini Rwanda,Mbali
na zawadi hiyo Mchezaji Nasra Suleiman wa Timu hiyo ya JWTZ ameshinda
tuzo ya Most Valuable Player (MVP) na hivyo kuongeza shangwe kwa T imu
ya Tanzania.
Akitoa
tuzo hizo ni Mkuu wa Jeshi la Anga la Rwanda Brigedia Generali Charles
Karamba alisema katika mashindano haya ambayo ushiriki ndio jambo muhimu
kwani sote ni washindi lakini wapo waliofanya vizuri wanaopaswa
kupongezwa.
Alisema
Katika Netball Tanzania imefanya Vizuri ikifuatiwa na Uganda kisha
Kenya hivyo ni nafasi nzuri kuwapongeza waliofanya vizuri zaidi na pia
waliofanya vibaya ili kujipanga upya katika mashindano yajayo.
Akizungumza
na Waadishi wa habari mkuu wa Msafara wa Timu za Tanzania na Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Timu za Tanzania Brigedia Jairos Mwaseba
aliipongeza Timu hiyo na kuda ushindi huo waliutarajia kutokana na
maandalizi yaliyofanyika.
Kwa
upande Mlinzi wa Timu hiyo Joyce Kaira na Mshambuliaji Mwanaidi Hasan
walisema wamefurahi kwani waliupoteza ubingwa huo mwaka jana.
Naye
Nahodha wa Timu hiyo Dorita Mbunda alisema maandalizi mazuri
yaliyofanywa na Jeshi ndio siri ya ushindi huo sambamba na Nidhamu na
kujituma.
Timu
hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kombe katika sherehe za ufungaji wa
mashindano hayo katika uwanja wa amahoro ambapo mchezo wa mwisho wa Soka
kati ya Rwanda na Tanzania utachezwa na kuamua mshindi wa mchezo huo.
Comments
Post a Comment