Salama: Nilimdis MwanaFA, Akanimaindi Kinoma!
UKIAMBIWA
umtaje Muasisi wa Kipindi cha Planet Bongo cha EATV ambacho enzi
ana-kifanya kilicha-ngia ubora wa video za Muziki wa Bongo Fleva nchini
kukua kutokana na kasumba yake ya kuzikosoa bila woga, moja kwa moja
utamtaja Salama Jabir ‘EceJay’.
Pia ukikutana naye, Salama ni mcheshi,
mtundu na ana ufahamu mkubwa katika masuala ya burudani. Kama ulishawahi
kufuatilia Vipindi vya Mkasi, Ngazi kwa Ngazi na Shindano la Bongo Star
Search (BSS) namna ya uulizaji wake wa maswali kimtego utaku-baliana
nami.
Mwi-shoni mwa wiki iliyo-pita, Salama
alifa-nyiwa maho-jiano katika Kipindi cha The Playlist cha Omary Tambwe
‘Lil Ommy’ kinachorushwa kupitia Radio Times FM na katika makala haya
yanaanika mahojiano hayo;
Ommy: Ngoma yako unayoikubali zaidi ni ipi?
Salama: Ahahaa! Jana
(Ijumaa) ujue nilikuandikia meseji, sasa nilikuwa nimeshiba kichizi na
nilikuwa nimekaa kwenye kikochi changu f’lan hivi cha tafakuru ambacho
ukikaa lazima madini yashuke! Nikakwambia nipigie Malome ya Cassper
Nyovest alioshirikiana na kikundi cha wamama wa kizamani sana wanaitwa
Mahotela Queens.
Ommy: Kwa nini unaikubali ngoma hii?
Salama: Ina ubunifu
uliopitiliza, ujue wasanii wengi wa Hip Hop wanapenda kufanya kazi na
wanamuziki wa R&B au wanamuziki wenzao wa Hip Hop. Wiki mbili tatu
zilizopita nilienda Sauz na AY nikakutana na hawa wamama, huwezi amini
Ommy, hawajui kabisa Kiingereza maana niliwafuata na kuwaambia nawapenda
nimekuwa nikiwaona tangu wanakua, sasa baadaye meneja wao (Mzungu)
alinifuata na kuniambia; ‘ulikuwa unaongea nini maana wanakudiskasi’
ndiyo nikajua kumbe hawakunielewa.
Ommy: Umegusia Sauz, kule ulienda kufanya nini?
Salama: Nilikuwa na AY
ambaye alienda kupafomu kwenye shoo moja ya uwanjani ya bure, wenzetu
huwa wanafanya sana kwa makampuni makubwa kurudisha kwa jamii. Kulikuwa
na wasanii wakubwa kutoka Afrika na pia ilikuwa inakaribia bethidei ya
Mandela.
Ommy: Hamkuingiza vitu maana sehemu kama hizo za fursa?
Salama: Yeah jambo lilikuwepo, nilikuwa na AY na Hermy B hivyo siyo vizuri nilizungumzie sana maana wenyewe wapo watalizungumzia.
Dah nimekumbuka Ommy, hongera bwana kwa kufunga ndoa, umechukua kitu nanii kabisa, hutaki kabisa kujifichaficha!
Ommy: Ahahaa! Ujue Insta na Facebook zilikuwa nyingi sana mara Tambwe vipi, baby sijui nini!
Turejee kwenye swali, tumeona upo karibu
sana wa AY na ikumbukwe kuwa AY ni mshkaji sana wa FA, lakini zamani
mshkaji wako wa karibu sana alikuwa FA na ukaribu wako na FA
ukasababisha kujuana na AY.
Salama: Dah! Yaani
umenipeleka mbali kishenzi, kwangu huwa sina za kubondibondi, kama ni
mshkaji wangu ni mshkaji na kama siyo siyo tu. Ujue mimi kuwa rafiki na
mtu ni ngumu sana na urafiki huwa unatoka kwenye roho, tangu nimekua,
marafiki zangu miaka nenda rudi ni haohao (AY na FA) na pia ni marafiki
kibiashara.
Ommy: Ulikuwa mkosoaji sana video za Kibongo, unafurahia video za sasa?
Salama: Nafurahi kuona
tumetoka sehemu moja kwenda nyingine na tupo mbali ukilinganisha kwa
nchi nyingine kwa maana ukiangalia wanavyoimba na ukiangalia video zao
duh, sijui wapo dunia ya wapi.
Ommy: Vitu gani haviko sawa katika video za Kibongo?
Salama: Kama
nilivyosema, kwanza inabidi tujikubali kwa hatua tuliyofikia. Ubunifu ni
suala lingine, tusikariri sana utakuta video jamaa amekutana na demu
akanunua nyanya.
Ommy: Unakumbuka nini katika kukosoa kwako?
Salama: Nakumbuka
ilikuwa Video ya Nakomaa Nao, mimi nikachambua kuwa FA hakupiga pasi
suti yake, dah kuna siku nilikuwa nimesha-sahau nikakutana nao pande za
Morocco nikasa-limiana nao lakini FA akani-chunia. Baada ya siku kadhaa
nikakutana na AY akaniambia jamaa alinichunia kwa kuwa nilimsema kwenye
video hajapiga pasi.
Comments
Post a Comment