Prof. Lipumba Akana Kuhusika na Vurugu Mkutano wa CUF
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amesema
kuwa hausiki na vurugu zilizoibuka katika mkutano mkuu wa chama hicho
uliovunjika juzi Jumapili, Agosti 21, wakati wa uchaguzi wa kujaza
nafasi zilizo wazi.
Akieleza hayo jana Jijini Dar es Salaam,
Prof. Lipumba amekiri kuwa hakualikwa katika mkutano huo lakini
aliombwa na baadhi ya wajumbe kwenda kutoa maelezo ya kwanini aliachia
nafasi hiyo ya uenyekiti jambo ambalo viongozi waliokuwepo ukumbini hapo
hawakulitaka.
Prof. Lipumba amesema kuwa anaheshimu
maamuzi ya pande zote mbili kwa wanaomtaka arejee nafasi ya uenyekiti
lakini pia maamuzi ya chama endapo utaratibu utafuatwa kwa kufuata
katiba ya chama na demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.
Prof. Lipumba amekataa kuhusika na
kukana kutumika na kisiasa na baadhi ya watu ili kukivuruga chama hicho
na kusema kuwa viongozi wa chama hicho waepuke maneno ambayo yataweza
kukigawanya chama hicho na badala yake wajikite katika kudumisha
demokrasia ndani ya chama hicho.
Comments
Post a Comment