MAALIM SEIF AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA MAREKANI
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sheriff Hamad akiwapungia
mkono baaadhi ya wananchama waliofika uwanja wa ndege zanzibar kumpokea
akitokea Marekani.
Maalim
Seif Shari Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF
akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika uwanja wa ndege wa
Kimataifa Abeid Aman Karume kumpokea. (Picha na Talib Ussi).
Na Talib Ussi, Zanzibar
Katibu
Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amerejea Nchini
leo akitokea katika ziara zake za Ughaibuni amewataka wanachi na
wanachama wa chama hicho kuendelea kuwa na subra.
Maalim ameyaeleza hayo nyumbani kwake wakati akitoa salamu kwa wananchgama waliokua kusanya hapo na kuomba kuelezwa chochote.
“Tumekutana
na watu muhimu katika safari yetu na imekuwa na mafanikio makubwa
lakini ni mapema kuwaeleza nini kinaendelea” alieleza Maalim Seif.
Alisema
kuwa katika safari yake hiyo amepokewa vizuri na kueleza matatizo ya
kubakwa kwa demokrasia Zanzibar na wote aliokutana nao alidai
wamemfahamu.
“Ni vyema tukaendelea kuwa subra huku mambo yetu yakifuatiliwa kwa karibu mnoo” alieleza Maalim Seif.
Malim
Seif alifika Kiwanja cha ndege Zanzibar munamo saa 11;30n za jioni
akiongozana na wajumbe ujumbe wake na walinzi wake waliandamana katika
ziara yake hiyo.
Mapema
baadhi ya viongozi wa chama hicho walifika kiwan jani hapo kwa ajili ya
kumpokea wakiongozwa na aliyekuwa Mgombea mwenza wa Ukawa Juma Duni
Haji.
Akimkaribisha
Maalim Seif Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Salim Biman alimueleza
maalimu kwamba wanancha leo walijipanga kuja kumpokea mapokezi makubwa
lakini alidai waliwazuia.
“Tumewaambia muda ukifika watakuja kumpokea kwa kishindo lakini kwanza watulie” alieleza Biman
Katika
ziarav hiyo Maalim Seif alienda Uengereza, Ubeligiji, Uholanzi na
baadae kuhudhuria mkutano Mkuu wa chama cha Democratic wa kumteua
mgombea wao Hilary Clinton huko Marekani.
Comments
Post a Comment