Chadema Wasitisha Maandamano ya UKUTA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kisitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike nchi nzima kesho Septemba Mosi yaliyopewa jina la UKUTA.
Akitangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa
Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa, wamefanya mazungumzo na
viongozi mbalimbalia wakiwemo viongozi wa dini, BAKWATA, Baraza la
Maaskofu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Taasisi ya Mwalimu
Nyerere na Jukwaa la Katiba na Jukwaa la wahariri na kuona wana kila
sababu ya kusikiliza ushauri huo.
Aidha, maandamano hayo yameahirishwa kwa mwezi mmoja ili kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka wa hali ya kisiasa nchini.
Comments
Post a Comment