Waziri Mkuu aongoza Swala ya Eid El Fitr jijini Dar
WAZIRI Mkuu wa Tanzania,
Majaliwa Kassim Majaliwa mapema leo Jumatano, ameongoza waumini wa dini
ya kiislamu katika swala ya Eid El Fitr iliyofanyika kwenye Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waumini mara baada ya
swala hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka waislamu wote nchini
kusherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya matendo mema ya kumpendeza
Mwenyezi Mungu.
Amewataka waumini wote kuwaombea dua
maalum watu waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyopoteza maisha
ya abiria 30 iliyotokea juzi Jumatatu mkoani Singida.
Naye Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh
Abubakary Zubery amewaomba waumini wa dini hiyo na wakristo kukaa pamoja
na kula pamoja, kusherehekea sikukuu hiyo ikiwemo kutoa sadaka kwa
wagonjwa na wasiojiweza.
Aidha Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhadi Mussa Salum naye alitoa nasaha zake kwa waumini wote wa
kiislamu kwa kufikisha siku ya leo ya mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani na kuwataka wanaoendelea kwa kufunga sita wawe na mfungo
mwema.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
Post a Comment