Rais Magufuli avunja rekodi ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amevunja rekodi baada ya kutangazwa
kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa kupata asilimia
100 ya kura zote zilizopigwa.
Rekodi hiyo ya kupata asilimia 100 ya
kura zote kwenye uchaguzi wa aina hiyo (Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
Taifa) haijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote ndani ya CCM tangu
kuanzishwa kwa chama hico Februari 5, 1977 ambapo ni miaka 39 sasa.
Wenyeviti wa CCM waliyopita ambao ni
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William
Mkapa wala Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete hawakuwahi kupata kura zote
zilizopigwa kwenye uchaguzi wa ngazi hiyo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo
uliyofanyika mjini Dodoma leo, Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake,
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema matokeo kuwa; ifuatavyo
Kura zilizopigwa zilikuwa ni 2398, kura halali ni 2398, kura zilizoharibika ni 0, kura za hapana ni 0 na kura za Ndiyo ni 2398.
Baada ya kumtangaza mshindi, Dkt.
Kikwete alimkabidhi Mwenyekiti mpya Dkt. Magufuli nyaraka za uongozi na
baada ya hapo Dkt. Kikwete alitangaza kustaafu rasmi Uenyekiti wa CCM na
kumuachia Dkt. Magufuli aongoze kwa miaka mitano ijayo.
Comments
Post a Comment