NITAHAKIKISHA SERIKALI INAHAMIA DODOMA :RAIS MAGUFULI
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi Rais Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe
wa mkutano mkuu maalum wa CCM uliofanyika mjini Dodomabaada ya
kuchaguliwa kwa kupigiwa kura za kishindo leo, kulia anayecheka ni
Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mzee Benjamin Williamo Mkapa..
Na. Immaculate Makilika- Dodoma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema
katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi
yake mjini Dodoma.Amesema
hayo leo, wakati alipokuwa akihutibia wajumbe wa Chama cha
Mapinduzi(CCM) katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama hicho uliofanyika
mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.“Nitahakikisha
katika awamu ya uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi
wengine wote nao watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma
inaweza kukidhi mahitaji yote” alisema Rais Magufuli.Rais
Magufuli aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi nane ya
uongozi wake chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ameweza kutekeleza
ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuanza kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili wananchi.Akiongelea
maeneo ya utekelezaji katika kipindi chake Dkt. Magufuli alisema kuwa
mpaka sasa Serikali imefanikiwa kusimamia suala la utoaji wa elimu bure
kwa shule za Msingi na Sekondari nchini na kuwezesha udahili kuongezeka
zaidi tofauti na miaka iliyopita.Aidha
Dkt. Magufuli alisema kuwa Serikali yake pia imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali hali itakayosaidia
kuimarisha utoaji wa huduma muhimu za jamii.Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imeagiza ndege mbili mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini Septemba mwaka huu,Rais
Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake kwa kushirikiana na Serikali
ya Uganda wamefanikiwa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima
katika ziwa Alberti nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga ambapo mafuta
hayo yatasafirishwa sehemu mbalimbali duniani na bombahilo litazalisha
zaidi ya ajira 20,000.Vile
vile, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali yake imeweza kurudisha
nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma na kuweza kuondoa watumishi hewa
waliokuwa na waliokuwa wamefikia 12,500,na kuongeza kuwa kwa mwaka huu
Serikali imetenga fedha za matumizi jumla ya shilingi trilioni 29.5,
ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitapelekwa katika kutekeleza shughuli
za maendeleo.Mkutano
Mkuu Maalum wa CCM ulihudhuriwa na wajumbe zaidi 2,000 ulimpitisha
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Chama hicho
kwa kura 2398 kati ya kura 2398 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia
100.Rais
Magufuli anakuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano baada ya kupokea uongozi
huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayemaliza muda wake Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 10.
Comments
Post a Comment