MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA JUMAPILI VIWANJA VYA SINZA-UZURI
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto),
mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi
na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga,
aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati
wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016
ulipowasili kutoka nchini India. MarehemuSenga alifariki katikati ya
wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa
marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili
asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na
kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na
marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu
utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA
NA K0-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili
Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa
Othmani
Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa
Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na
marehemu Senga
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili
Mbunge wa
Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri
Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel
Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta
jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena,
wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa
mpiga picha mkuu wa gazeti hilo
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka
Comments
Post a Comment