Cameron Kuachia Ngazi Leo Uingereza
David Cameron .
Theresa May leo anakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke katika historia ya nchi ya Uingereza baada ya Margaret Thatcher
aliyetumikia nafasi hiyo kati ya 1979-1990. Waziri mkuu huyo mtarajiwa
huenda akaongeza nafasi nyingi zaidi za wanawake kwenye baraza la
mawaziri. Mwanamama Amber Rudd huenda akateuliwa katika moja ya nafasi
nyeti ya waziri wa mambo ya ndani au waziri wa fedha.
Justine Greening.
Justine Greening na Priti Patel waliokuwa vinara wa kutaka nchi ya
Uingereza kujitoa kwenye Jumuiya ya Ulaya wanapewa nafasi kubwa ya
kuteuliwa na waziri mkuu mpya anayeamini umefika wakati wa wanawake
kupewa majukumu zaidi katika nafasi nyeti ndani ya serikali.
Priti Patel.
Waziri mkuu mtarajiwa anaweza kuvunja rekodi ya kuwateua wanawake wanane kwenye baraza lake la mawaziri.Leo asubuhi waziri mkuu aliyejiuzulu atawasilisha barua kwa Malkia Queen Elizabeth II itayohitimisha utawala wake na kutoa nafasi ya kuundwa kwa serikali mpya ya May.
Comments
Post a Comment