Mrembo Anayedaiwa Kutembea na Diamond Kumbe Denti
Mrembo anayedaiwa ‘kutembea’ na Diamond, Irene Hilaly ‘Lynn’.
Stori: Mayasa Mariwata, RISASI JUMAMOSI
BINTI anayedaiwa kubanjuka kimalovee na staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’ anayejulikana kwa jina la Irene Hilaly ‘Lynn’ kumbe ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msimbazi Centre aliyeacha masomo akiwa kidato cha tatu mwaka jana.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika,
Irene anayeonekana katika video ya Wimbo Kwetu wa Raymond, anadaiwa kuwa
na umri chini ya miaka 18, hajahudhuria shuleni tangu Machi mwaka jana
na endapo angekuwa akienda, hivi sasa angekuwa kidato cha nne.
“Kila kukicha walimu wanawatuma
wanafunzi wenzake wamtafute Irene sababu hawajui pa kumpata, ili tu
arudi shule aendelee na masomo kwa kuwa tangu alipofanya mtihani wa
kidato cha pili akawa anakuja kwa kusuasua mwisho akakata mguu kabisa
‘form three’ mwanzoni,” kilisema chanzo hicho.
Staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo paparazi
wetu alifunga safari hadi ilipo shule hiyo maeneo ya Ilala jijini Dar na
kufanikiwa kuzungumza na walimu kadhaa, ambao walionesha masikitiko yao
kwa kitendo chake cha kukacha shule.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo Ahobwile Msimba alisema angependa kumuona na kuzungumza naye ili amalizie masomo yake.
“Tangu kidato cha kwanza kasomo hapa na
alikuwa binti mwenye tabia nzuri, kwani mama yake alikuwa akimfuatilia
sana maendeleo yake ila baada ya kufariki ndo balaa likaanza, kundi lao
walikuwa wanne wote wakawa wanakuja wanapojisikia. Irene alikuwa anavaa
sketi ndefu na hijabu ghafla akabadilika na kuanza kuvaa kisketi kifupi
na hijabu akaacha,” alisema mwalimu huyo.
Hata hivyo, alisema mwanafunzi huyo hakuwa na maendeleo mazuri shuleni na kwamba hiyo ilimsaidia kuvuka kuingia kidato cha tatu kutokana na kufutwa kwa utaratibu wa mitihani ya kidato cha pili.
Hata hivyo, alisema mwanafunzi huyo hakuwa na maendeleo mazuri shuleni na kwamba hiyo ilimsaidia kuvuka kuingia kidato cha tatu kutokana na kufutwa kwa utaratibu wa mitihani ya kidato cha pili.
“Anatupa wakati mgumu kwa kasi hii ya
Magufuli sababu hakutoa taarifa kama kaacha au la, tumekuwa tukimtafuta
kwa kipindi kirefu, mara tukaanza kumuona kwenye televisheni na
magazeti, tupo tayari aje aendelee na kidato cha nne ili apate cheti
kimsaidie maishani maana hata miaka 18 hajafika, au huyo Diamond
atusaidie kumpata tuzungumze naye.”
Juhudu za kumpata Irene ziligonga mwamba ila shushushu wetu alifanikiwa kumpata kaka yake ambaye ndiye meneja wake, aliyejitambulisha kwa jina la Sammy Hilaly ambaye alikiri mdogo wake kusoma shule hiyo na kusitisha masomo kwenda kujiendeleza nchini Afrika Kusini.
“Kifupi ni kwamba pale aliacha na kwenda
kusoma kozi huko Sauz na ameshamaliza masomo yake,” alisema bila
kufafanua elimu aliyosomea
Juhudu za kumpata Irene ziligonga mwamba ila shushushu wetu alifanikiwa kumpata kaka yake ambaye ndiye meneja wake, aliyejitambulisha kwa jina la Sammy Hilaly ambaye alikiri mdogo wake kusoma shule hiyo na kusitisha masomo kwenda kujiendeleza nchini Afrika Kusini.
Comments
Post a Comment