RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLAI OVA) ENEO LA TAZARA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kuashiria ufunguzi
rasmi na kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua jiwe la msingi kwa ajili
ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua ramani ya mradi wa
barabara ya juu eneo la Tazara kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa
ujenzi wa mradi huo Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea maelekezo kuhusu mradi wa
barabara za juu eneo la Tazara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wakala wa
barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale katika ufunguzi rasmi wa
mradi huo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka
jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika
makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara Jijini Dar es
salaam ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018.
Sherehe
ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika kando ya eneo la makutano ya
barabara ya Nyerere na Mandela Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na
Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, imehudhuriwa
na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Mameya wa Jiji la Dar
es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida.
Barabara
hiyo ya juu itakuwa ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake
umepangwa kugharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha
hizo shilingi Bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika lake la
Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi
Bilioni 8.3.
Barabara
ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutokea
maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano
wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es
salaam.
Akizungumza
kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Rais Dkt. John Pombe
Magufuli amesema barabara hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi
ya serikali yake ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar
es salaam, ambao kwa mwaka 2013 pekee utafiti umeonesha ulisababisha
upotevu wa shilingi Bilioni 411.55
Rais
Magufuli amebainisha juhudi nyingine za kukabiliana na msongamano wa
magari Jijini Dar es salaam kuwa ni pamoja na kujenga barabara ya njia
sita ya Dar es salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na Flyover tano,
ujenzi wa barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson
Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo na ujenzi wa daraja
jipya la Salander lenye urefu wa kilometa 6.23 kuanzia Coco Beach hadi
hospitali ya Agha Khan.
Juhudi
nyingine ni ujenzi wa awamu ya pili wa miundombinu ya mabasi yaendayo
haraka katika barabara za Kilwa, Chang'ombe na Kawawa, na ujenzi wa
awamu ya tatu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara
za Nyerere - Gongo la Mboto na Uhuru - Azikiwe.
Aidha,
Rais Magufuli amezungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi yaendayo
haraka, kuwa serikali yake imelazimika kusimamisha kuanza kwa huduma
hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo
zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa
mzigo mzito wa viwango vikubwa vya nauli, na amewahakikishia wananchi wa
Dar es salaam kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma hivi karibuni
baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika.
Dkt.
Magufuli pia amezungumzia usafi wa Jiji la Dar es salaam kwa kuwataka
viongozi wa Manispaa zote za Jiji, kuhakikisha wanatafuta namna ya
kudhibiti utupaji hovyo wa takataka ikiwemo kutoza faini kubwa kwa
watakaokamatwa wakitupa takataka hovyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Aprili, 2016
Comments
Post a Comment