MWANAFUNZI MTANZANIA ASHIRIKI ONYESHO LA UBUNIFU LILILOANDALIWA NA RAIS BARACK OBAMA
.Oh
"Kumbe kinafanya kazi hivi" ndivyo anavyoelekea kusema Rais Obama mara
baada ya kuweza kukiendesha kifaa hicho kwa kutumia simu, aliyechuchuma
ni Stephen Mwingira ambaye pamoja na Wendy Ni na Armon Halwan walipata
fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika onyesho la mwisho lililoandaliwa
na Rais Barack Obana na kufanyika White House April 13. 2016.
.Mwanafunzi
Armo Halwan akimuelekeza Rais wa Marekani,Barack Obama anavyoweza
kutumia simu kuendesha cha kufanyia usafi ( Vacuum Cleaner)
kilichobuniwa na wanafunzi wa Baruch Collage Campus High School ya
Jijini New York kupitia timu yao ya ufumbuzi (Invent Teams)katikati ni
Wendy Ni na anayefuatia ni Stephen Mwingira ( mtanzania) anaonyesha
namna gani kifaa hicho kinavyofanya usafi kwenye njia za treni za
ardhini ( Subways).
Stephen
Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini jinsi Rais Obama
anavyoelekezwa namna ya kutumia simu kuendesha mashine hiyo katika
Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack
Obama katika Ikulu ya Rais ( White House Science Fair 2016)
Rais Barack Obama akipeana mkono na Stephen Mwingira na timu yake
baada ya kumaliza kutoa maelezo yao kifaa walichokibuni. Kwa miaka sita
Rais Barack Obama amekuwa akifadhili maonyesho ya ubunifu wa vifaa
mbalimbali vilivyobuniwa na wanafunzi kuanzia wale wa shule za wali
hadi sekondari ikiwa ni jitihada zake za kuwahamasisha wanafunzi
kupenda masomo ya sayansi, teknolojia na hesabu tangu wakiwa wadogo na
hivyo kuibua vipaji vyao. katika onyesho hilo la mwisho wa utawala wa
Barack Obama jumla ya wanafunzi 130 kutoka states mbalimbali
walishiriki.
Stephen
Mwingira akiendelea kutoa maelezo zaidi kwa Rais Obama namna kifanya
cha kufanyia usafi kwenye njia za reli ambacho ni cha gharama nafuu
kinavyofanya kazi.
April
13, 2016, Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili onyesho la
mwisho katika utawala wake, onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja
za sayansi ambalo limewahusisha wanafunzi kuanzia shule
za awali,msingi hadi za sekondari kutoka States mbalimbali
za Marekani.
Kwa
miaka sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa
akifadhili onyesho hilo lijulikanalo kama White House Science
Fair ambalo limekuwa likifanyia katika Ikulu yake (White House)
lengo likiwa ni kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya
sayansi, hisabati ,teknolojia na ufundi ( STEM)na
hivyo kuibua vipaji vya ubunifu mwiongoni mwa wanafunzi ( young
inventors) .
Katika
onyesho hilo la Aprili 13 jumla ya wanafunzi 130 walishiriki baada
ya kukidhi vigezo vya kuingia katika onyesho hilo. Miongoni mwa
wanafunzi waliopata fursa hiyo adhimu ya kushiriki baada ya kukidhi
vigezo ya ubunifu wao ni mwanafunzi mtanzania Stephen Wilfred
Mwingira ambaye pamoja na wenzake wawili Armo Halwah na Wendy
Ni wanaosoma Baruch College Campus High School ya jijini New
York, wamebuni kifaa cha gharama nafuu ( vacuum cleaner) kinachoweza
kutumika katika kusafisha njia za reli za chini ya ardhi (
Subways).
Stephen
Mwingira na timu yake, walipata fursa ya kuelezea na kuonyesha
mbele ya Rais Obama namna gani kifaa walichobuni ( Vacuum Cleaner)
kinavyoweza kufanya usafi kwa kufungwa kwenye treni na hivyo
kusaidia katika kuzifanya njia za treni ( subways) kuwa
katika mazingira ya usafi na hivyo kupunguza gharama za usafishaji.
Katika
miaka sita tangu Rais Obama ambaye yeye binafsi amejipambanua kama
mpenzi na shabiki mkubwa wa sayansi na ubunifu, onyesho hilo limekuwa
motisha na kivutio kikubwa kwa walimu, wanafunzi, wafadhili
na wataalamu waliobeba katika masuala ya sayansi, teknolojia
na hesabu.
Kila
mwaka State dining room ya Ikulu hugeuzwa kuwa eneo la
maeonyesho ambapo wanafunzi hujipanga na kuonesha vifaa walivyobuni
au kutoa maelezo ya kisayansi ya namna ya kutatua tatizo Fulani kwa
kutumia teknolojia nafuu.
Katika
kutambua mchango wa Rais Barack Obama katika kuwahamasisha
wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, Ikulu ya White
House imetangaza kwamba Kampuni ya Oracle inayojihusisha na masuala ya
teknolojia ya Komputa katika miezi kumi na nane ijayo itawekeza dola
za kimarekani 200 milioni kwaajili ya masomo ya sayansi ya
computa kwa wanafunzi wa kimarekani.
Katika
maelezo yake kwa vyombo vya habari kabla na baada ya kuhitikishwa kwa
onyesho lake la mwisho, Rais Barack Obama amesema, mara zote ambazo
ameshiriki kujionea ubunifu wa vijana hao wadogo na wenye kiu na ari ya
kuibua mambo mapya, amekuwa akijifunza kitu kipya na mara zote
amejiona kama anayepungukiwa na kitu kutokana kile anachojifunza
kutoka kwa wanafunzi hao.
Comments
Post a Comment