Tungeshangilia Filamu za Bongo Kama Tulivyofanya Kwa Ray na Hadithi yake ya Maji na Weupe Wake, Tungekuwa Mbali
Ray
alitengeneza headlines sana hivi karibuni kwa kauli yake kuwa weupe
wake umetokana na kunywa maji mengi. Story ilikuwa viral na ilisambaa
kwenye mitandao yote.
Watu walianza kupost picha wakinywa maji kuutafuta weupe kama wa Ray kama njia ya kumtania kwa kauli yake hiyo. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini muigizaji huyu alikuwa gumzo kama hivi. Hadi kuna tetesi kuwa kutokana na kauli yake kusambaa kwa ukubwa usioelezeka, makampuni ya maji yanataka yampe mchongo.
Hatua hiyo ilinifanya nianze kujiuliza maswali mengi. Ni lini Ray amekuwa midomoni kwa watu kwa filamu aliyoifanya? Ni kwasababu Ray ana filamu yake mpya iitwayo Tajiri Mfupi ambayo ajabu haizungumzwi kama inavyozungumzwa kauli yake hiyo ya maji na weupe wake.
Utasema kuwa filamu za Bongo sio nzuri ama hazina viwango kama za nje lakini kumbe tunawafahamu waigizaji hawa na tunawafuatilia. Tunapenda kujua maisha yao lakini hatupendi kuangalia filamu wanazofanya.
Kwahiyo huenda wachawi wa filamu za Tanzania ambazo zinadaiwa kuanza kudoda, ni sisi wenyewe. Tunafawahamu sana wasanii hawa lakini hatutaki kuunga mkono kazi zao.
Pale wanapotoa kauli za kama za weupe kusababishwa na kunywa maji mengi tunapagawa! Vipi kama tungekuwa na mwamko kama huu wa kusambaza filamu wanazotoa akina Ray? Nadhani tungesaidia kuinyanyua tasnia hii inayopumulia mashine.

Comments
Post a Comment