Simba kushuka kijeshi, Kaseja azua hofu Mbeya City

simba_muda
Wachezaji wa Simba wakifanya yao.
Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
BAADA ya kuwa mafichoni kwa takriban wiki moja mkoani Morogoro, kikosi cha Simba sasa kipo fiti, tayari kuwavaa Mbeya City katika mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Simba-Day-559x520
Simba wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya lakini Simba ilikuwa chini ya Muingereza, Dylan Kerr wakati kwa sasa ipo chini ya Mganda, Jackson Mayanja.
Meneja wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amewahakikishia Wanasimba kuwa kwa mazoezi waliyofanya, wana uhakika wa ushindi.
“Kikosi kipo vizuri, bahati nzuri wachezaji karibia wote wapo, isipokuwa Hija Ugando ambaye alibaki Dar akiuguza majeraha, lakini wengine wote wapo kambini katika maandalizi ya mchezo huo,” alisema Gazza.
Juma-KasejaF.jpg
Kipa wa Mbeya City, Juma Kaseja.
Aidha, upande wa Mbeya City, kikosi chao kimekuwa kikiwasili Dar kimafungu ambapo kundi moja la wachezaji tayari lilitua Dar, jana wakati kundi jingine litashuka kesho, hii ni kwa mujibu wa ofisa habari wao, Dismas Ten. Kupitia tovuti ya klabu hiyo jina la kipa mkongwe, Juma Kaseja halikuwemo katika orodha ya wanaotarajiwa kuwemo kwenye kikosi kitakachocheza Jumapili, huku kipa huyo akionekana jijini Dar tangu mwanzoni mwa wiki hii.
Taarifa zinasema kuwa Kaseja hatakuwemo katika kikosi hicho lakini alipoulizwa Ten alisema: “Hilo ni jukumu la kocha kuamua nani wa kucheza.”

Comments

Popular posts from this blog