Ray C, Hali Tete

RAY-C-3-(1)  
Rehema Chalamila ‘Ray C’ baada ya hali kuwa tete (picha na maktaba).

MUSA MATEJA, AMANI
DAR ES SALAAM:
Hali ya mrembo aliyekuwa akifanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kabla ya kutopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, Rehema Chalamila ‘Ray C’, si shwari kwani sasa amerudishwa kwao, Bunju jijini Dar hivyo kuzua wasiwasi wa jinsi atakavyoweza kutumia dawa, tembea na Amani.
ray-c4Chanzo cha uhakika kilichopo ndani ya idara ya tiba katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, kimesema mrembo huyo hali yake ya kiafya inatishia amani baada ya siku chache zilizopita kukaidi utumiaji wa dawa za kuondoa sumu akiwa hospitalini hapo hivyo kurudishwa kwao.
“Ndugu yangu nimeamua kukuita ili kukusimulia kwa kirefu hali ya huyu mrembo ilivyokuwa baada ya kurudia tena matumizi ya dawa za kulevya na maendeleo yake.
“Kwanza Ray C ameanza kuongea maneno yasiyoeleweka na mengine unajua kabisa hana uhakika nayo ingawa anasema kama ana uhakika,” kilisema chanzo hicho huku maneno hayo yakihifadhiwa na gazeti.
ray-c1Ray C katika pozi.
Chanzo: “Karibu watu wote walioteuliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na mimi nikiwa mmoja wao kwa ajili ya kusimamia tiba ya huyu dada tumekata tamaa hivyo tukaamua arudishwe kwao. “Hapa hospitali aliletwa Februari 14, mwaka huu.
Tukaendelea kumhudumia lakini juzi tulifikia hatua ya kumrudisha nyumbani kwao kutokana na yeye kutotoa ushirikiano kwa watoa huduma wake.”
Gazeti hili liliwasiliana na meneja wa muziki wa Ray C, Ruge Mutahaba ambaye alikiri mrembo huyo kurudishwa kwao bila kuongeza zaidi.
Juzi, mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa akina Ray C kwa lengo la kutaka kuongea naye au mama yake lakini mtu aliyefungua geti aligoma kutoa ushirikiano.
Gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda la Februari 22, mwaka huu, liliandika habari ya staa huyo kufungiwa hospitalini hapo kwa lengo la kumfanya amudu kutumia dozi katika mtiririko unaotakiwa kitabibu. Habari hiyo ilikuwa na kichwa; RAY C AFUNGIWA HOSPITALI.
source:GPL

Comments

Popular posts from this blog