ORODHA KAMILI YA WAHANGA WA AJALI LEO KATIKA AJALI BARABARA YA MANDELA
Ajali
mbaya sana asubuhi hii barabara ya Mandela eneo la karibu na Daraja la
Matumbi. Haitazamiki baada Roli lililokuwa limebeba ng’ombe kuvaana
uso kwa uso na daladala Toyota DCM linalofanya safari zake katika ya
Gongo la Mboto na Ubungo limefyekwa lote Taarifa kutoka kwa Stanley
Binagi Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana zinasema zilipokelewa
maiti 3 kutokana na ajali hiyo na majeruhi walikuwa 26 hata hivyo
majeruhi mmoja alifariki mara baada ya kusikishwa hospitali ya Amana na
kufanya idadi ya waliokufa katika ajali hiyo kufikia 4 huku baadhi ya
majeruhi wakihamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Foleni
ilikuwa ni kubwa sana na jitihada za kuyatoa magari hayo kutoka kikosi
cha usalama barabarani zilifanyika na kupunguza foleni katika barabara
hiyo.
Baadhi ya Ng’ombe walionusurika kwenye ajali wakitapakaa hovyo barabarani mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Haya ndiyo mabaki ya daladala hilo.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani akitekeleza majukumu yake mara baada ya ajali hiyo.
Comments
Post a Comment