WAZIRI KITWANGA AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI, AWATAKA WAPANGE MIKAKATI MIPYA YA KUPAMBANA NA WAHALIFU NCHINI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya kufungua Mkutano wa
Mwaka wa Jeshi hilo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa
hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na
Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na
uhalifu nchini. Watatu kulia meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Polisi
(IGP), Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake kwa
Maafisa Waandamizi wa Jeshi lake, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) kuzungumza na maafisa hao
kutoka mikoa yote nchini na kuufungua Mkutano wao wa Mwaka unaofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es
Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga kabla ya kufungua mkutano
huo, aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali
ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu
nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimshukuru
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB nchini, Ineke Bussemaker, mara baada ya
kumkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia),
Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya kuudhamini Mkutano wa Mwaka wa Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa yote nchini. Mkutano huo
ulifunguliwa na Waziri Kitwanga katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, na aliwataka Maafisa hao
kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia
wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.
Sehemu
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, wakimsikiliza mgeni
rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alipokuwa
anazungumza na maafisa hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam kabla ya waziri huyo kuufungua
Mkutano huo wa Mwaka wao wa Mwaka kwa ajili ya kufanya tathimini ya
utendaji wao pamoja na kuliboresha zaidi Jeshi hilo. Katika hotuba yake,
Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya
kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange
mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiyajibu maswali
mbalimbali ya waandishi wa habari ambao walitaka kupata ufafanuzi zaidi
kutokana na hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake,
Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana
na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana
na uhalifu nchini. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments
Post a Comment