RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI ARUSHA KUONGOZA MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru
Msshariki Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi na wananchi
waliojitokeza kwa wingi kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida
wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utofanyika jijini
Arusha.
Picha na IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda mara baada
ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
,Kikanda na Kimataifa Balozi Agustine Mahiga mara baada ya Kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

akizungumza na wakazi wa Arusha na Kilimanjaro waliofika Uwanja wa ndege
wa KIA kumpokea.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege
wa Kimatifa wa Kilimanjaro (KIA). PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………….
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili
Mkoani Arusha ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa
kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
utakaofanyika Jumatano tarehe 02 Machi, 2016 Mjini Arusha.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli
amelakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja
na vikundi vya burudani za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.
Rais
Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Kabla
ya kuongoza kikao hicho Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya
mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Tarehe
03 Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe
la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha – Holili –
Taveta – Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.
Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
02 Machi 2016
Comments
Post a Comment