Picha 15: Cheka alivyomkalisha Mserbia

CHEKA NA MSERBIA (1) CHEKA NA MSERBIA (2) CHEKA NA MSERBIA (3) CHEKA NA MSERBIA (4) CHEKA NA MSERBIA (5) CHEKA NA MSERBIA (6) CHEKA NA MSERBIA (7) CHEKA NA MSERBIA (8) CHEKA NA MSERBIA (9) CHEKA NA MSERBIA (10) CHEKA NA MSERBIA (11) CHEKA NA MSERBIA (12) CHEKA NA MSERBIA (13) CHEKA NA MSERBIA (14) CHEKA NA MSERBIA (15)

Bondia Francis Cheka ‘SMG’ jana usiku alifanikiwa kuiandikia Tanzania historia nyingine mpya baada ya kumchapa Muingereza, Geard Ajetovic katika pambano la kugombania Ubingwa wa mabara (WBF Intercontinetal).
Katika pambano hilo la raundi 12 lililopigwa kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Cheka alioneka kucheza kwa uwoga mkubwa kitendo kilichopelekea kuangushwa nchini kwenye raundi ya kwanza tu kufuatia makonde makali kutoka kwa Ajetivic ambaye alikuwa amepania kumaliza pambano mapema kabisa.
Mashabiki wengi waliokuwa kwenye Viwanja vya Leaders walionekana kuwa na hofu kutokana na Ajetovic kuachia ngumi kali za kushitukiza ingawa Cheka alipiga nyingi zaidi za kudokoa zilizomsaidia kupata pointi nyingi.
Lakini kadiri mchezo unavyosonga mbele, kidogo akaanza kuonyesha cheche na kubadilika ingawa mpinzani wake aliendelea kupiga ngumi kali huku raundi ya tisa, Cheka akichanika na kuanza kuvuja damu, lakini bado alionekana kuwa mvumilivu na kuendelea kupambana akiwa amepania kulipa kisasi.
Hata hivyo ushindi alioupata Cheka umelalamikiwa na Ajetovic kwa madai ya kuwa amependelewa licha ya yeye kucheza vizuri zaidi ya Cheka
source.GPL

Comments

Popular posts from this blog