OMBAOMBA TISHIO ANAYEOMBA KWA KUTUMIA KISU IRINGA .


Askari polisi  mjini Iringa akiwa ameshika kisu baada ya kufanikiwa  kumnasa kijana Mohamed Iddy (18) mkazi  wa mjini Iringa kutokana na kutishia maisha ya  wakazi wa mji  wa Iringa akiwa katika  shughuli yake ya kuomba hudaiwa  kuhatarisha maisha ya  wananchi kwa  kuwafukuza kwa kisu pindi anaponyimwa pesa ,
Kijana  huyo  omba  omba tishio akipelekwa  kituo cha polisi pamoja na kisu anachotumia kutishia  wananchi  wakati  akiomba  pesa 
Askari  polisi  wakiwa  wamembana   lilivyo  kijana   huyo omba omba 


Hapa  akiwa  eneo la  Miyomboni akipelekwa  kituoni 




OMBA  omba  hatari anayeomba kwa nguvu kwa kutumia kisu kwa wananchi  wanaomnyima msaada  wa  pesa amekamatwa na jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa  kufuatia msako mkali  dhidi  yake.

Tukio  la kukamatwa kwa  kijana   huyo lilitokea leo majira ya saa 5 asubuhi katika  eneo la Posta  mjini Iringa baada ya  kuwepo kwa malalamiko mengi  kutoka kwa  wananchi wa mji wa Iringa  hasa  wanawake ambao  wamekuwa  wakifukuzwa kwa kisu na kijana  huyo omba omba baada ya kumnyima  pesa.

Mmoja kati ya  wanawake ambao  wamepata   kutishiwa  kuchomwa  kisu na kijana  huyo aliyetajwa kwa jina la Mohamed Iddy  Chengula (18) Bi Amina Said mkazi wa Mkwawa alisema  kuwa ni  zaidi ya  mara  mbili amenusurika  kuchomwa  kisu na  kijana  huyo omba omba .

Alisema  kuwa mji  wa Iringa una omba omba  wengi ila mbinu hiyo anayotumia kijana Mohamed ya  kutembea na  kisu na  kuomba kwa kutishia  kisu ni mpya  kutokea mjini hapa na ni omba omba  pekee ambae kwa mwonekano haonyeshi kama ni omba  omba anaonyesha ni kijana mtanashati mzuri ila vitendo vyake  ndivyo  vimekuwa tishio kubwa kwa  wananchi.

Huku  vijana  wauza magazeti  eneo la  Posta  walidai kuwa ni mara  kadhaa  wamekuwa  weakishuhudia  mbinu chafu  za  kijana   huyo ambazo wao  wanafananisha na unyang'anyi na  sio omba omba  wa kawaida .

Kwani   walisema  haiwezekani kama ni omba  omba  kweli  kutembea na  kisu na pindi anaponyimwa pesa anachomoa kisu na  kutaka  kumchoma yule  aliyemnyima  pesa na  wakati  mwingine huwafukuza hasa  wanawake .

Vijana   hao  walisema  tukuo  la leo kwa omba  omba   huyo  kutishia  kumchoma mtu  kisu mbele ya askari  hao  ndilo ambalo  limefanikisha  kukamatwa  kwake .

Hata   hivyo  askari  hao walionyesha ukomavu  mkubwa wa  kiaskari katika  kumkamata  ombaomba   huyo ambae alikuwa akitishia  kuwachoma  kisu kabla ya  kumdhibiti kisawa  sawa na kumpeleka  kituo cha  polisi.

Kamanda  wa polisi mkoa wa Iringa Peter Kakamba pamoja na kuthibitisha  kutokea kwa  tukio hilo alitaka  wananchi  kutoa ushirikiano kwa  jeshi la polisi pindi  wanapoona matukio ya  watu kama  hao kwani ni hatari katika jamii

Comments

Popular posts from this blog