Linah: Mastaa Afrika wananitaka kimapenzi
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’.
Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu staa wa Muziki wa Bongo Fleva,
Estalina Sanga ‘Linah’ aachane na mchumba wake, amekiri kutakwa
kimapenzi na mastaa wa muziki nje ya nchi (Afrika).Akichonga na Amani Linah amesema, mara nyingi amekuwa akisumbuliwa kimapenzi na mastaa wengi wa muziki Afrika lakini hakuwa tayari kuwaweka wazi na wala kutaja kama alishawahi kubanjuka na mmoja wapo kati ya hao.
“Ni kweli wapo wengi walionitaka kimapenzi, lakini itabaki kuwa siri yangu kujua ni wangapi na nilimkubalia nani kati ya hao,” alisema Linah.
Comments
Post a Comment