USIYOYAFAHAMU KUHUSU FIRST LADY MAMA JANETH MAGUFULI
Kila
mzazi anapokaribia kupata mtoto, moja ya mambo muhimu ambayo hufikiria
juu ya jina la kumpatia baada ya kujifungua na mtoto kuishi duniani.
Wazazi
wengi huchukua muda kufikiria ni jina gani zuri la kumpa mtoto wao.
Kuna wakati baadhi ya wazazi hufikia hatua ya kuvutana kuhusu jina tu.
Kuvutana huko kunatokana na umuhimu wa jina kwa sababu inaaminika kila jina lina maana yake na tabia zake zitaakisiwa nalo.
Kuna
majina ambayo hupendwa sana kutokana na dhana kwamba watu wanaopewa
majina hayo huwa na tabia nzuri, upeo mkubwa, uvumilivu na wengine
bahati.
Je,
ikitokea unabahatika kupata mtoto wa kike uliyemtafuta kwa muda mrefu,
utampa jina gani? Huenda jina Janeth likawa miongoni mwa matatu au 10
utakayoorodhesha ili kuchagua moja la kumpa binti yako.
Kama halitakuwapo basi fanya mpango wa kuliweka kwa sababu jina hilo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
Kwa
nini jina la Janeth ni habari ya mjini? Siku Dk John Magufuli
alipopitishwa na CCM kuwania nafasi ya urais, baadhi ya watu walidai
ikiwa angepata nafasi hiyo Afrika Mashariki ingeongeza idadi ya wake wa
marais wenye majina ya Janeth.
Imekuwa
hivyo, mke wa Rais Magufuli aliyeapishwa jana anaitwa Janeth. Mke wa
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anaitwa Janet Museveni, na mke wa
Rais wa Rwanda, Paul Kagame anaitwa Jeanette.
Licha ya kwamba jina la mke wa Kagame linaandikwa tofauti na mengine, lakini matamshi ya majina hayo ni sawa.
Kwa
mujibu wa kamusi ya Encyclopaedia jina la Jeannette, asili yake ni
Ufaransa ndiyo maana linaandikwa tofauti na Janeth ambalo asili yake ni
Scotland.
Kama hujui wakati jina Janeth hupewa mtoto wa kike kinyume cha jina hilo ambao hupewa mtoto wa kiume ni John.
Kwa
hiyo majina ya Janeth na John Magufuli yameshabihiana vilivyo. Kutokana
na utuki huo majina ya wake za marais hao sasa yamekuwa habari ya
mjini.
Kuna baadhi ya watu wanatamani kuwapa majina watoto wao kwani huenda wakawa ‘ma First Lady’ watarajiwa.
Gumzo kwa sasa au watu wengi wanahoji iwapo marais hao watakutana wakiwa na wake zao, likataitwa jina hilo, itakuwaje?
Maana
ya jina Janeth Kwa mujibu wa kamusi ya tafsiri ya majina, jina Janeth
(Kiebrania) ambalo asili yake ni Uingereza linamaanisha Mungu ni mwenye
neema.
Sifa
za wanawake wenye jina hilo zimedadavuliwa zaidi na tovuti ya
‘sevenreflections’. Tovuti hiyo inawaelezea wanawake wenye jina hilo
kuwa ni waaminifu, wema, wenye vipaji na wavumbuzi wa mambo.
Wanawake
wenye majina hayo ni jasiri, wavumilivu, wabunifu, wadadisi, wanafahamu
nini wanataka, siyo tegemezi na viongozi wazuri.
Janeth
Magufuli Kitaaluma ni mwalimu. Alikuwa anafundisha Shule ya Msingi
Mbuyuni masomo ya Jiografia, Historia na Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA).
Lakini
ameacha kutokana na wadhifa huo mpya aliopata mumewe. Hata hivyo,
hakuwa maarufu wakati alipokuwa anafundisha shuleni hapo licha ya kuwa
mke wa waziri mchapakazi na sasa rais.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo, Dorothy Malecela anamzungumzia kama mwalimu
mchapakazi na anayefahamu majukumu yake, mwenye upendo, mnyeyekevu na
asiye na makuu, sifa ambazo zinaendana na jina lake.
Janet
Museveni Licha ya kuwa Mke wa Rais Museveni tangu mwaka 1986 mumewe
alipoingia madarakani, pia ni mwanasiasa, na ni Waziri wa Karamoja.
Jeannette
Kagame Alipata wadhifa wa mke wa rais tangu mwaka 2000, Kagame
alipoingia madarakani hadi sasa akiwa pia mwanaharakati, mwanzilishi wa
taasisi ya Imbuto inayosaidia katika shughuli za maendeleo katika sekta
ya afya, elimu na uchumi.
Mwanamke mwingine maarufu duniani mwenye jina hilo ni Janeth Jagan, aliyekuwa Rais wa Guyana kati ya mwaka 1997 na 1999.
Comments
Post a Comment