MWANAMKE ASHAMBULIWA KWA KUZUNGUMZA KISWAHILI MAREKANI
Mwanamke aitwaye, Asma Jama ameshambuliwa nchini Marekani kwa kuongea Kiswahili.
Jama
alikuwa amekaa na familia yake kwenye mgahawa wa Applebee huko
Minnesota, akikata kiu na juice huku mazungumzo yakiendelea kabla ya
kujeruhiwa vibaya mdomoni. Mwanamke aliyekuwa amekaa jirani yake
alimponda na glasi nzito ya bia mdomoni.
Sababu? Jama alikuwa akizungumza Kiswahili na familia yake.
“Siamini
baada ya miaka yote hii mtu ananipiga sababu niko tofauti,” alisema
Jama. “Mtu ananipiga kwasababu nilikuwa nikizungumza lugha ya kigeni.”
Shambulio lilimwacha Jama na majeraha usoni pamoja na mdomo kuchanika kiasi cha kushonwa nyuzi 17.
Jodie
Burchard-Risch, 43, na mume wake, walikuwa wamekaa kwenye mgahawa huo
jirani na Jama, aliyekuwa ameketi na binamu na watoto wa nduguze. Wawili
hao walichukizwa baada ya kumsikiliza Jama na familia yake wakizungumza
lugha ngeni.
Jodie Burchard-Risch
Jama alisema wawili hao waliwaambia waende nyumbani. “Walisema ukiwa Marekani unatakiwa kuzungumza Kiingereza.”
Jama, ambaye ni msomali, alihamia Minnesota mwaka 2000 kutoka Kenya. Anazungumza lugha: Kiingereza, Kiswahili na Kisomali.
Jumatatu hii, Burchard-Risch alishikiliwa kwa kosa la shambulio.
Kutokana
na shambulio hilo, Jama anadai hana amani tena na anafikiria kuhama
Minnesota. Amesema anaweza kuungana na dada yake aliyehama Minnesota
mwezi June na kwenda Dallas.
Comments
Post a Comment