Rais Kikwete Ateua Wakuu wa Mikoa Wawili,Mganga Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na
wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK),
Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete
amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu
Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Aidha,
Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa – Ndugu Mwantumu Bakari
Mahiza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga na Ndugu Saidi Magalula ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
akitokea Mkoa wa Tanga.
Ndugu Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma pia.
Ndugu
Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Morogoro na
Naibu Waziri wa Maji anachuku anafasi iliyoachwa wazi na ndugu Leonidas
Gama ambaye anawania ubunge mkoani Ruvuma.
Ndugu
Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro anakuwa Mkuu wa
Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Mahiza.
Uteuzi
na uhamisho huo ulianza Jumamosi, Septemba 12, mwaka huu, 2015 na wakuu
wapya wa mikoa wataapishwa Jumatano, Septemba 16, 2015, Ikulu, Dar es
Salaam.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Profesa Muhammed Bakari Kambi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Taarifa
iliyotolewa Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK),
Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Jumatano,
Septemba 9, 2015.
Kabla
ya uteuzi wake, Profesa Muhammed Bakari Kambi alikuwa Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Tiba na Afya Shirikishi cha Muhimbili, Dar es Salaam.
Vile
vile, Rais Kikwete amemteua Ndugu Mlingi Elisha Mkucha kuwa Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC). Uteuzi huo ulianza
Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.
Taarifa
iliyotolewa Jumatatu, Septemba 12, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK)
Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa Ndugu Mlingi Elisha Mkucha ni
mwanasheria kwa taaluma na mwajiriwa wa NDC kwa miaka 14 iliyopita
ambako ametumikia katika nafasi mbali mbali mpaka akawa Kaimu Mtendaji
Mkuu.
Ndugu Mkucha anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Gideon Nassari aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.
Wakati
huo huo, Rais Kikwete amemteua Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali kuanzia Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Tulia Ackson ni Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Comments
Post a Comment