Mgombea Mwenza Urais CCM Azungumza na Wanachama UWT Dodoma
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi.
Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa
CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata
heshima hiyo
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika
mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu
ya CCM Dodoma.

heshima hiyo.

ya CCM Dodoma.[/caption] MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amefanya mazungumzo na wanachama wa
Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kuitumia vema heshima na
nafasi waliopewa akinamama nchini ya kushika nafasi ya makamu wa rais
kwa mara ya kwanza, hivyo kuhakikisha wanahamasisha wenzao ili CCM iweze
kushinda na wanawake kutwaa heshima hiyo. Bi. Suluhu amesema hayo
alipokuwa akizungumza na akinamama wa UWT mkoani Dodoma ikiwa pamoja na
kutaja kipaumbele ambapo kimewekwa kwa akinamama katika ilani mpya ya
CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Alisema atatumia
nafasi yake kushawishi akinamama kipata vifaa na mazingira rafiki ya
kuendesha kilimo cha kisasa ili waweze kukuza uchumi wao, pia
kuwawezesha katika vikundi vya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na kukomesha
usumbufu ambao akinamama wafanyabiashara wamekuwa wakibughuziwa na
mgambo wa jiji. Mgombea huyo alisema kupitia vikundi akinamama
watawezeshwa na fungu la fedha shilingi milioni hamsini fedha ambazo
zitatolewa kila kijiji maalumu kwa ajili ya kuwawezesha akinamama pamoja
na vijana ili waweze kukuza mitaji yao. Pamoja na hayo Bi. Suluhu
alisema Serikali watakayoiunda itashughulikiwa changamoto anuai
wanazokumbana nazo walemavu hasa akinamama ili kuwawezesha na wao katika
ushindani. "...Kwa upande wa kilimo nitahakikisha nachochea kidogo
kidogo ili wanawake wapate vitu kama pembejeo na vifaa vingine
kuwawezesha kuendesha kilimo cha kisasa," alisema.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Ummy Mwalimu
akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM
(UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.[/caption]
[caption id="attachment_61330" align="aligncenter" width="691"]
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM (mbele)
walioambatana na mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu wakiwa katika mkutano
na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika Ukumbi wa NEC
ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma
Mke wa waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na
wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kabla ya mkutano huo na
mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi.
Samia Suluhu jana kuanza katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya
CCM Dodoma.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Asumpta
Mshana akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa
CCM (UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, Bi. Salome
Kiwaya akizungumza kabla ya mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya
urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana kuanza katika
Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika
mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu
ya CCM Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_61327"
align="aligncenter" width="800"]
Baadhi ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa
Wanawake wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika
mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu
ya CCM Dodoma
Makundi ambalimbali ya akinamama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT)
mkoani Dodoma, wakimpa zawadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi.
Samia Suluhu katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM
Dodoma.[/caption] Alisema ilani ya CCM imetoa kipaumbele kwa huduma za
afya hasa huduma za mama na mtoto ikiwa ni kutambua changamoto na
matatizo wanayokumbana nayo akinamama eneo hilo. Alisema atadhibiti
rushwa na matumizi mabaya ya dawa zinazopelekwa wizara ya afya
kuhakikisha zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kudhibiti urasimu.
Aliongeza kuwa baada ya ujenzi wa shule za kata kufanikiwa akiingia
madarakani anaongeza nguvu katika ujenzi wa mabweni ya wasichana ili
kukabiliana na changamoto ya mimba kwa wanafunzi wasichana ambazo
zimekuwa zikichangiwa na wao kutembea umbali mrefu na kupata changamoto
njiani. Aidha aliongeza kuwa ili kuonesha Serikali ya CCM inawajali
walimu itaunda chombo maalumu ambacho kitakuwa na kazi ya kushughulikia
matatizo ya walimu pamoja na kukiwezesha kuhakikisha kinatimiza majukumu
yake kiufasaha. Aliwaomba akinamama kushirikiana kufanya kampeni na
kuhakikisha CCM inashinda hivyo akinamama kupata fursa hiyo waliyopewa
na CCM kwa sasa. "...Naombeni tushirikiane wote kufanya kampeni nyumba
kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka ili kuhakikisha
tunashinda maana hii ni zawadi kwa akinamama tujitahidi tuweze kushinda
nafasi hii," alisema Bi. Suluhu.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika
mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu
ya CCM Dodoma
Baadhi ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa
Wanawake wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika
mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu
ya CCM Dodoma.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika
mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu
ya CCM Dodoma.[/caption] *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Comments
Post a Comment