DK.SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad
Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi sana tangu mgombea wa
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama
hicho. Leo ameibuka na kusema ya moyoni kuwa amejivua uanachama rasmi
wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama cha hicho na
kuaachana kabisa na siasa kutokana na mambo yaliyokuwayakifanyika ndani ya chama chake hayakumlidhisha na hakukubaliana nayo.
Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad
Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndio maana
ameamua kuachana na siasa rasmi hii leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad
Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es
salaam leo.
Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment