Wanachama zaidi ya 500 wa CHADEMA wahamia ACT...Kadi Zachomwa Moto Laivu

Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.
Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.


Wanachama hao wamefikia maamuzi ya kukihama chama hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga.
Mamia ya wanachama hawa kutoka wilaya ya Ludewa, wamefanya maandamano ya amani kutoka mtaa wa Kilimahewa hadi katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Ludewa wakiwa na mabango ya aina mbalimbali yakilaani viongozi wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata Okol Haule aliyeshinda katika kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.


Hata mara baada ya wanachama hawa kuwasili katika ofisi za CHADEMA wilaya, viongozi waliingia mitini na kufunga ofisi, lakini dhamira ya wafuasi hawa wa CHADEMA wakiwemo viongozi wa juu kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Ludewa, haikuishia hapo na wote wakiwa hawana imani tena na CHADEMA wakaelekea ofisi za ACT Wazalendo mtaa wa Sokoni na kujiunga nacho.
Huku wakidhamiria kuisambaratisha kabisa CHADEMA wilayani humo, wanachama hao wakiungana na mgombea wao wanayemuhitaji bwana Okol Haule wakachoma moto nguo aina ya kombati alizokua akizitumia mgombea huyo, bendera na kadi za CHADEMA ambapo bwana Haule anasema ameshindwa kuvumilia ubakaji wa demokrasia uliofanywa na viongozi wa CHADEMA.

Comments

Popular posts from this blog